Sep 04, 2023 04:45 UTC
  • Arsenal yaigaragaza Manchester United 3-1

Timu ya soka ya Arsenal ya Uingereza jana iliendeleza matokeo mazuri ya msimu huu wa Ligi Kuu ya EPL baada ya kuwatandika watani wao wa jadi Manchester United mabao 3 kwa moja la kufutia machozi.

Vijana wa Gunners ambao timu yao inaundwa na makinda waliuanza mchezo huo kwa kasi ya ajabu huku wakkitandaza soka la kisasa. Wangeweza kupata mabao ya haraka mapema lakini walichezea nafasi walizokuwa wakipata.

Upepo ulikwenda kinyume kabisa na jinsi mchezo ulivyokuwa ukienda kwani licha ya Arsenal kushambulia goli la Mashetani Wekundu kama nyukil lakini walijikuta wakipachikwa bao na Marcus Rashford katika dakika ya 27 ya mchezo. Hata hivyo, wakati mashabiki wa Machester United wakiwa hawajamaliza kushangilia, Gunners walisawazisha dakika moja baadaye kupita kwa nahodha wake kijana Martin Odegaard.

 

Hadi mapumziiko mambo yalikuwa nguvu sawa. Kipindi cha pili kilishuhudia Arsenal wakikosa nafasi za wazi huku Manchester United wakiweka ukuta wakionekana kuridhika na sare. Wakati mashabiki wengine wakiwa wameshatoka uwanjani wakidhani matokeo ni sare vijana wa Arsenal walipachika mabao ya haraka haraka katika dakika za nyongeza kupitia Declain Rice na Gabriel Jesus na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3 kwa 1.

Katika mechi zingine zilizopgwa jana katika Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza,  Bwawa la Maini Liverpool waliigaragaza Aston Villa mabao matatu kwa yai, huku Cystal Palace wakiilaza Wolvae kwa mabao matatu kwa mawili. Nchini Uhispania wikii ya nne ya ligi kuu ya ka nchini humo LALIGA ilimazika kwa wababe Barcelona kuitandika Osasuna mabao mawili kwa moja, Athletic Bilbao ikitoka suluhu ya bila bila na Mallorca huku Las Palmas ikichezea kipigo cha bao moja kwa yai mbele ya Girona.

Tags