Sep 16, 2023 02:25 UTC
  • Jenerali Mark Milley
    Jenerali Mark Milley

Mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerali Mark Milley amekiri kuwa vita ilivyoanzisha nchi hiyo huko Afghanistan vimeishia kwa kushindwa vikosi vya jeshi hilo.

Milley amekiri kwamba kuondolewa kwa majeshi ya nchi yake nchini Afghanistan kulikuwa ni kushindwa kimkakati na akabainisha kuwa vita vya miaka 20 vilivyoendeshwa na Marekani nchini Afghanistan vilimalizika kwa kushindwa Washington.

Katika mazungumzo na televisheni ya ABC News kuhusiana na kuondolewa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, Jenerali Mark Milley amesema "vita vyetu vya miaka 20 nchini Afghanistan havikuwa na mafanikio yoyote".

Wanamgambo wa Taliban

Kamanda huyo mkuu wa majeshi ya Marekani ametoa tathmini jumla kuhusu matokeo ya vita vya nchi hiyo huko Afghanistan kwa kusema: "Kwa maana pana zaidi, vita vilishindwa. Tulipigana na Taliban na washirika wao kwa zaidi ya miaka 20. Wao walipata ushindi Kabul kwa sababu nyingi".

Huku akikiri kushindwa kwa Washington nchini Afghanistan, Mkuu wa majeshi ya Marekani ameelezea namna majeshi hayo yalivyoondoka nchini humo kuwa nako pia ni kushindwa kimkakati, japokuwa rais wa Marekani Joe Biden amejaribu mara kadhaa kutetea uamuzi wake juu ya suala hilo.../

 

Tags