Marekani yahamisha silaha zilizopigwa marufuku kutoka Ujerumani kwenda Ukraine
(last modified Sun, 28 Jul 2024 08:04:00 GMT )
Jul 28, 2024 08:04 UTC
  • Marekani yahamisha silaha zilizopigwa marufuku kutoka Ujerumani kwenda Ukraine

Vyombo vya habari vya Ujerumani vimefichua kuwa nchi hii inahifadhi mabomu yaliyopigwa marufuku ya vishada ya Marekani na kwamba inapanga kuyahamishia Ukraine.

Kanali ya redio na televisheni ya Ujerumani (NDR) imetangaza kuwa Marekani inatumia eneo la Berlin kama mahali pa kupakia na kuhamishia mabomu ya vishada nchini Ukraine, na kutaja hatua hiyo kuwa ni ukiukaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN) unaopiga marufuku silaha hizo.

Kulingana na Mkataba wa Umoja wa Mataifa ulioidhinishwa mwaka 2008, zaidi ya nchi 110 zimepiga marufuku mabomu ya vishada. Sababu ya kupigwa marufuku  mabomu ya vishada  ni kuwa yanasababisha hatari na maafa makubwa kwa raia wa kawaida.

Ufichuzi wa vyombo vya habari vya Ujerumani kuhusu uhamisho wa silaha zilizopigwa marufuku za Marekani kutoka Berlin hadi Ukraine

Wakati huo huo, msemaji wa Kamandi ya Marekani barani Ulaya na Afrika amesema kuwa silaha za Marekani zinazohifadhiwa katika ghala la silaha la nchi hii katika mji wa Miesau, Ujerumani Magharibi zinatumwa nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa msemaji huyo, mabomu hayo ya milimita 155 M864 na M483A1 ni miongoni mwa silaha ambazo zinahifadhiwa katika kambi ya kijeshi ya Marekani mjini Miesau.

Viongozi wa Ujerumani wamekataa kabisa kuzungumzia suala hilo.