Canada: Tuko tayari kujibu vitisho vya ushuru vya Trump
-
Mélanie Joly
Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada amesema kuwa nchi hiyo imejiandaa kujibu hatua yoyote ya Washington ya kuiwekea Canada ushuru mpya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada ameeleza haya siku chache kabla Rais mteule wa Marekani, Donald Trump hajaanza kazi rasmi katika Ikulu ya White House.
Mélanie Joly Waziri amesema: Kwa kuzingatia kwamba asilimia 75 ya bidhaa za Canada zinauzwa nchini Marekani, kuzidishwa ushuru kwa bidhaa hizo kunaweza kusababisha hasara ya kiuchumi kwa nchi hiyo.
Joly ameongeza kuwa: "Tuko tayari na tumejipanga kwa ajili ya duru ya pili na ya tatu iwapo Rais wa Marekani ataanza kazi siku ya Jumatatu."
Waziri wa Nishati na Maliasili wa Canada Jonathan Wilkinson pia alithibitisha Alhamisi kwamba nchi yake inaweza kutoza ushuru kwa mauzo ya nje kwa madini muhimu.
Chombo kingine cha kuaminika pia Jumatano iliyopita kilieleza kuwa: Iwapo Trump atatekeleza tishio lake la kuzidisha ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Canada, nchi hiyo itachukua hatua haraka dhidi ya kundi dogo la bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani ikiwa ni pamoja na maji ya machungwa kutoka Florida, sehemu anayoishi Trump.