Utafiti: Francois Hollande kuwania tena urais Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i1462-utafiti_francois_hollande_kuwania_tena_urais_ufaransa
Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande huenda akatetea kiti chake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 18, 2016 04:28 UTC
  • Utafiti: Francois Hollande kuwania tena urais Ufaransa

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa, Rais wa Ufaransa, Francois Hollande huenda akatetea kiti chake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kanali ya televisheni ya BFM imesema asilimia 70 ya Wafaransa wanaamini kuwa Hollande atawania tena urais mwakani licha ya uongozi wake kukabiliwa na matatizo mengi. Utafiti huo pia unaonyesha kuwa, chama cha Kisosholisti kina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kikilinganishwa na chama cha mrengo wa kulia ambacho kina misimamo mikali.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, Rais Hollande amepata umaarufu kutokana na jinsi alivyoshughulikia mashambulizi ya kigaidi dhidi ya mji wa Paris miezi kadhaa iliyopita.

Hata hivyo, wakosoaji wa serikali ya Hollande wanasema kujihusisha Paris na mambo ya ndani ya nchi zingine na kufeli chama cha kisosholisti kukabiliana na wimbi la wahajiri haramu ni baadhi ya mambo yatakayofanya serikali ya sasa kupoteza kura nyingi kwenye uchaguzi huo.