Apr 22, 2017 03:43 UTC
  • Polisi ya Ufaransa: Mtekelezaji wa shambulizi la Paris alikuwa mhalifu sugu

Polisi ya Ufaransa imetangaza kuwa, mtu aliyehusika na shambulizi la jana mjini Paris alikuwa na historia ya uhalifu na kufungwa jela.

Taarifa iliyotolewa na Polisi ya Ufaransa imesema kuwa, mtu aliyefanya shambulizi la Alkhamisi usiku katikati ya jiji la Paris ambaye pia aliuawa, ni mwanaume aliyekuwa na umri wa miaka 39 kwa jina la Karim Cheurfi ambaye alishawahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la kuua watu watatu wakiwemo maafisa wawili wa polisi.

Polisi ya Ufaransa imeongeza kuwa, mhalifu huyo aliachiwa huru kwa masharti mwaka 2015. 

Ufyatuaji wa risasi uliotokea Alkhamisi usiku katika mtaa wa Champs-Élysées mjini Paris umesababisha mauaji ya maafisa wawili wa polisi na mtu alifanya shambulizi hilo. Shambulizi hilo pia limejeruhi watu wengine kadhaa. 

Kundi la kigaidi na kiwahabi la Daesh limetangaza kuwa ndilo lililofanya shambulizi hilo. 

Tags