Chomsky: Marekani inaelekea kwenye maangamizi
Mwanafikra mashuhuri wa Marekani, Noam Chomsky amesema nchi hiyo inaelekea kwenye maangamizi kutokana na fikra za uliberali na mfumo mpya wa soko.
Noam Chomsky amesema Marekani inakabiliwa na tishio la kusambaratika na kwamba inaelekea kwa kasi kwenye maangamizi mabaya kutokana na mfumo mpya wa soko. Ameeleza kuwa, kuelekea kwenye uliberali mpya kunalipa soko sio jamii nguvu ya mamuzi yote na ametahadharisha kuwa, makampuni yanayofanya kazi katika mabara ya dunia na taasisi za kifedha sasa zinaongozwa na maslahi ya watu binafsi nchini Marekani.
Mwanafikra huyo wa Marekani ameongeza kuwa, kinyume na inavyopigiwa debe kwamba uliberali mpya unapanua uhuru wa Wamarekani, fikra hizo zinaimarisha dhulma na ukandamizaji.
Amesema kuwa, watu wanaokosoa fikra za uliberali mpya nchini Marekani wanapachikwa jina la "maadui wa Marekani" na kuongeza kuwa, hizi ni sifa za tawala za kidikteta.
Noam Chomsky amekikosoa chama tawala cha Rebuplican nchini Marekani na kusema kuwa, kinafanya jitihada za kuharibu maisha ya watu. Amesisitiza kuwa Marekani inaelekea kwenye maangamizi katika kipindi cha sasa ambapo walimwengu wanafanya jitihada za kurekebisha hali hiyo.