Jul 08, 2017 02:52 UTC
  • Wanachama UNESCO wakataa wito wa kukaa kimya dakika moja kwa sababu ya Holocaust

Wito uliotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kikao cha Shirika la Elimu, Syansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wa kunyamaza kimya dakika moja ili kuonesha heshima kwa eti wahanga wa mauaji ya Holocaust umekabiliwa na upinzani mkali wa mwakilishi wa Cuba katika kikao hicho.

Ripoti zinasema mwakilishi wa Cuba katika shirika la UNESCO amekosoa vikali jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya taifa la Palestina na kusema: Ni lazima kunyamaza kimya dakika moja ili kuonesha heshima kwa Wapalestina wanaoendelea kuuawa na Israel (na si kwa ajili ya Holocaust).

Matamshi hayo ya mwakilishi wa Cuba katika shirika la UNESCO yameshangiliwa na kuungwa mkono na wawakilishi wa nchi nyingine walioshiriki kikao hicho.

Ngano ya kile kinachodaiwa ni mauaji ya Wayahudi katika Vita vya Pili vya Dunia (Holocaust) inafungamana na falsafa ya kuanzishwa dola bandia la Israel katika ardhi ya Palestina na ni marufuku kujadili au kutilia shaka madai hayo katika nchi za Magharibi. 

Nchi za Magharibi pia zimewapiga marufuku wasomi kufanya utafiti na uchunguzi kuhusu madai hayo ya eti kuuawa maelfu ya Mayahudi katika Vita vya Pili vya Dunia, suala ambalo linazidisha ukweli kwamba, ni ngano isiyokuwa na mashiko wala msingi.  

Tags