Ongezeko la Chuki dhidi ya Waislamu Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i31954-ongezeko_la_chuki_dhidi_ya_waislamu_marekani
Kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jul 18, 2017 21:58 UTC
  • Ongezeko la Chuki dhidi ya Waislamu Marekani

Kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani.

Kwa mujibu wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), kampeni iliyojaa chuki ya Rais Trump wa Marekani ndiyo chanzo cha chuki dhidi ya Waislamu na jamii zingine za walio wachache nchini humo.

CAIR imesema, hilo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka 2016.

Kwa mujibu CAIR kumeripotiwa visa 940 vya chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu.

Maandamano ya kupinga chuki dhidi ya Uislamu

CAIR inasema Trump hajali maisha ya Waislamu nchini Marekani na ndiyo sababu ya kuongezeka vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Waislamu.

Trump ametia saini sheria za kibaguzi za kuwazuia raia wa nchi sita za Kiislamu kuingia Marekani. Ingawa sheria hiyo imepingwa vikali na mahakama lakini hivi sasa inatekelezwa na nukta hiyo imechangia ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu nchini Marekani.