Kuongezeka mpasuko ndani ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32152-kuongezeka_mpasuko_ndani_ya_serikali_ya_rais_donald_trump_wa_marekani
Katika hatua mpya inayodhihirisha mpasuko uliopo ndani ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani, Sean Spicer Msemaji wa Ikulu ya Rais wa nchi hiyo (White House) ametangaza kujiuzulu wadhifa wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2017 06:44 UTC
  • Kuongezeka mpasuko ndani ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani

Katika hatua mpya inayodhihirisha mpasuko uliopo ndani ya serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani, Sean Spicer Msemaji wa Ikulu ya Rais wa nchi hiyo (White House) ametangaza kujiuzulu wadhifa wake.

Kufuatia uamuzi huo, Anthony Scaramucci ambaye ameteuliwa na Trump kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa White House, amemuarifisha Sarah Huckabee Sanders kuwa msemaji mpya wa ikulu ya Rais wa Marekani. Hatua ya Trump ya kumuuzulu Sean Spicer kutoka cheo chake cha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa White Hiouse na kumteua Scaramucci kwenye nafasi hiyo, imedhihirisha wazi hitilafu kubwa zilizopo katika ikulu ya Marekani.

Sean Spicer, aliyepigwa kalamu nyekundu na kujiuzulu

Katika kulalamikia uamuzi huo, Spicer ameamua kujiengua kutoka nafasi ya msemaji wa White House, na kwa utaratibu huo mmoja kati ya wanachama wa timu kampeni ya Trump ambaye kiujumla hana uzoefu na masuala ya habari yaani Anthony Scaramucci ameteuliwa na rais huyo kusimamia kitengo cha mawasiliano cha ikulu hiyo.

Hata hivyo tangu hapo awali Rais Donald Trump hakufurahishwa na matamshi ya Spicer katika kutetea mienendo ya rais mbele ya vyombo vya habari vinavyomkosoa na kwa msingi kulikuwa kukisikika tetesi juu ya uwezekano wa kuuzuliwa kutoka cheo cha msemaji wa ikulu ya White House. Hatua hiyo ni moja ya mifano ya wazi ya kuwepo mpasuko mkubwa katika timu ya wafanyakazi wa ikulu ya Rais wa Marekani na hata serikali ya nchi hiyo kwa ujumla.

Anthony Scaramucci, aliyeteuliwa na Trump

Wakati huo huo, vyombo vya habari vya nchi hiyo vimefichua kuwa, Rais Trump na washauri wake, wanaizunguka Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Rex W. Tillerson, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, ili waweze kutekeleza siasa mpya kuhusiana na mudhui ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA. Inaelezwa kuwa, msimamo wa Wziara ya Mambo ya Nje ya Marekani wa kukiri kwamba, Iran imeheshimu kikamilifu makubaliano ya JCPOA, umemkasirisha sana Rais Donald Trump na washauri wake wenye misimamo mikali. Kadhalika ilielezwa kuwepo tofauti kubwa kama hizo kati ya White House na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuhusiana na mgogoro wa kisiasa kati ya Qatar na Saudi Arabia.

Makubaliano ya nyuklia yanayokiukwa na Marekani

Katika hali ambayo Trump ameungana na Saudia dhidi ya Qatar, Wizara ya Mambo ya Nje imetaka kufanyike usuluhishi kati ya pande mbili au kupunguzwe mgogoro baina ya nchi za eneo la kusini mwa Ghuba ya Uajemi. Hii ni katika hali ambayo, mbali na kuwepo tofauti kati ya Idara ya Wafanyakazi wa White House na kati ya viongozi wa ngazi ya juu wa baraza la mawaziri la Trump, vilevile kunashuhudiwa hitilafu kubwa ndani ya chama tawala cha Republican. Mfano wa hivi karibuni wa tofauti hizo ni hatua ya idadi kadhaa ya maseneta wa Republican kukataa kupitisha pendekezo la Trump la mpango mbadala wa sheria ya bima ya afya maarufu kwa jina la 'Obamacare' na kuifanya White House ifeli vibaya. Mkabala wake pia Rais Trump amewatishia maseneta wasiofuata siasa zake kwamba watapoteza nafasi zao katika uchaguzi wa kiduru wa kongresi mwaka ujao wa 2018.

Trump akiwa amechanganyiwa asijue la kufanya

Vitisho hivyo vya Trump dhidi ya maseta wa chama chake mwenyewe vinaweza kuchochea zaidi moto wa hitilafu zilizopo katika timu ya kiongozi huyo wa Marekani. Aidha kuendelea hali hiyo kutazidisha hitilafu ndani ya serikali na hivyo kumfanya Trump ashindwe kukabiliana na matatizo ya ndani na nje ya nchi, suala ambalo litakuwa na taathira hasi na hatari licha ya kujaribu kufunika na kupindisha fikra za walio wengi juu ya uwepo wa tofauti kubwa ndani ya serikali ya sasa ya Marekani