Watu 8 wapoteza maisha, 28 wajeruhiwa katika magendo ya binadamu Texas
https://parstoday.ir/sw/news/world-i32166-watu_8_wapoteza_maisha_28_wajeruhiwa_katika_magendo_ya_binadamu_texas
Maafisa katika jimbo la Texas nchini Marekani wametangaza kuwa miili ya watu wanane imepatikana ndani ya lori kwenye eneo moja la kuegeshea magari huko Saint Antonio jimboni humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2017 10:06 UTC
  • Watu 8 wapoteza maisha, 28 wajeruhiwa katika magendo ya binadamu Texas

Maafisa katika jimbo la Texas nchini Marekani wametangaza kuwa miili ya watu wanane imepatikana ndani ya lori kwenye eneo moja la kuegeshea magari huko Saint Antonio jimboni humo.

Polisi na kitengo cha zima moto katika eneo la Saint Antonio wameripoti leo kuwa miili ya watu wanane na watu wengine 28 waliojeruhiwa wamekutwa ndani ya lori huku hali za watu 20 zikiwa mbaya sana. Polisi wamesema kuwa wameanzisha uchunguzi ili kuusaka mtandao unaojihusisha na magendo hayo ya binadamu. Takwimu zilizotolewa mwaka jana zinaonyesha kuwa magendo ya binadamu nchini Marekani yameongezeka kwa asilimia 35.7 huku watu 7572 wakiwa wahanga wa magendo hayo ya binadamu. Wanawake 6340 ni miongoni mwa wahanga wa magendo hayo ya binadamu nchini Marekani kwa mujibu wa takwimu hizo za mwaka uliopita wa 2016. Majimbo ya California, Texas na Florida kwa utaratibu ndiyo yanayoongoza kwa  biashara hiyo haramu.

Takwimu za magendo ya binadamu Marekani  

Imeelezwa kuwa magendo ya binadamu nchini Marekani yana faida kubwa ya kifedha na wakati huo huo hatari yake ni ya kiwango cha chini; hivyo kuifanya kuwa moja ya sababu kuu zinazopelekea kuongezeka kwa jinai hiyo nchini humo.