'Ni unafiki US kusema itashirikiana na ICC dhidi ya ISIS'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i3373-'ni_unafiki_us_kusema_itashirikiana_na_icc_dhidi_ya_isis'
Mchambuzi mmoja mashuhuri wa masuala ya kisiasa amesema serikali ya Marekani haiaminiki na kwamba madai yaake ya hivi karibuni kwamba iko tayari kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuhakikisha wanachama wa kundi la kigaidi na kitaifiri la ISIS au Daesh wanapandishwa kizimbani ni ya kinafiki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 19, 2016 04:17 UTC
  • 'Ni unafiki US kusema itashirikiana na ICC dhidi ya ISIS'

Mchambuzi mmoja mashuhuri wa masuala ya kisiasa amesema serikali ya Marekani haiaminiki na kwamba madai yaake ya hivi karibuni kwamba iko tayari kushirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuhakikisha wanachama wa kundi la kigaidi na kitaifiri la ISIS au Daesh wanapandishwa kizimbani ni ya kinafiki.

Eric Draister ameiambia kanali ya televisheni ya Press TV kuwa, suala ambalo haliwezi kuangaziwa na vyombo vya habari vya Magharibi, ni ukweli mchungu kwamba, Marekani imekuwa ikiunga mkono harakati za ISIS na hivyo kusema kuwa iko tayari kusaidia uchunguzi dhidi ya kundi hilo la kigaidi na kitakfiri ni kichekesho. Machambuzi hiyo Mmarekani amsisitiza kuwa: “Huwezi kuwaacha wahalifu wakajichunguza wenyewe.” Ameongeza kuwa Washington na kundi la kigaidi na kitaifiri la ISIS zinatafuta lengo moja katika mapigano na mauaji ya kikatili huko Syria na Iraq.

Alkhamisi iliyopita, Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest alisema kuwa serikali ya Washington iko tayari kushirikiana na mahakama ya ICC eti katika ukusanyaji wa ushahidi juu ya jinai za kutisha zinazofanywa na Daesh.

Marekani na waitifaki wake wamehusika katika uanzishaji makundi ya kigaidi kama vile Al Qaeda na ISIS na kisha kushindwa kidhahiri kuyadhibiti makundi hayo ambayo sasa yanatekeleza jinai za kutisha kote duniani.