Macron: EU itaendelea kuheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i35839-macron_eu_itaendelea_kuheshimu_makubaliano_ya_nyuklia_ya_jcpoa
Rais wa Ufaransa amesema kuwa Ulaya inafanya kila liwezekanalo kulinda makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya kundi la 5+1 na Iran na kwamba yeye pia yuko tayari kuanza mazungumzo na Iran kuhusu miradi ya makombora na ushawishi wa nchi hiyo katika eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Oct 20, 2017 22:57 UTC
  • Macron: EU itaendelea kuheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

Rais wa Ufaransa amesema kuwa Ulaya inafanya kila liwezekanalo kulinda makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya kundi la 5+1 na Iran na kwamba yeye pia yuko tayari kuanza mazungumzo na Iran kuhusu miradi ya makombora na ushawishi wa nchi hiyo katika eneo la Mashariki ya Kati.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesisitiza mwishoni mwa kikao cha Baraza la Ulaya mjini Brussels Ubelgiji juu ya ulazima wa nchi za Ulaya kutekeleza vipengee vyote vya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kueleza kuwa, hii inamaanisha kuanza tena uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo na Iran na kujiepusha kuweka mashinikizo ya aina yoyote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.  

Rais Emannuel Macron wa Ufaransa akihutubia mkutano wa EU mjini Brussels 

Rais wa Ufaransa ameongeza kuwa, kuweka mashinikizo ni uamuzi wa Marekani unaopingana na suala la kulindwa makubaliano ya JCPOA. 

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe 13 mwezi huu alipuuzilia mbali ripoti zote nane zilizotolewa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) zinazosisitiza kwamba Iran imetekeleza majukumu yake kuhusu makubaliano ya JCPOA na kutishia kuwa, upo uwezekano nchi hiyo ikajiondoa katika makubaliano hayo ya kimataifa.

Umoja wa Ulaya na nchi nyingi duniani zimejibu matamshi hayo ya Trump zikisisitiza kuwa zitaendelea kutekeleza makubaliano hayo.