Uingereza yataka raia wake waliojiunga na ISIS Syria wauawe
https://parstoday.ir/sw/news/world-i35901-uingereza_yataka_raia_wake_waliojiunga_na_isis_syria_wauawe
Uingereza inataka raia wake waliojiunga na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh nchini Syria wauawe kabla ya kupata fursa ya kurejea nyumbani.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Oct 24, 2017 01:01 UTC
  • Uingereza yataka raia wake waliojiunga na ISIS Syria wauawe

Uingereza inataka raia wake waliojiunga na kundi la kigaidi la ISIS au Daesh nchini Syria wauawe kabla ya kupata fursa ya kurejea nyumbani.

Waziri wa maendeleo ya kimataifa wa Uingereza Rory Stewart amesema Waingereza waliojiunga na ISIS si watiifu tena kwa serikali ya nchi hiyo na ni hatari kubwa kwa usalama wa Uingereza. Amesema wafuasi wa kundi la kigaidi la ISIS wanafuata itikadi yenye chuki kubwa sana.  Stewart amesema: "Ni lazima tufahamu kuwa, watu hawa ni hatari kwetu sisi na njia pakee ya kukabiliana na kila mmoja wao ni kuwaua."

Matamshi ya Stewart yamekuja baada ya Brett McGurk, mjumbe wa ngazi za juu wa Marekani katika muungano wa nchi za Magharibi unaodai kupambana na ISIS katika nchi za Iraq na Syria kudai kuwa, jukumu lake sasa ni kuhakikisha kuwa wapiganaji wote wa kigeni wa ISIS wanauawa nchini Syria.

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Rory Stewart

Katika miezi ya hivi kairbuni, Uingereza imelengwa na magaidi kadhaa wa kundi la ISIS. Taarifa zinasema kuna raia 850 wa Uingereza ambao wamesafiri Syria na Iraq na kujiunga na makundi ya magaidi wakufurishaji katika nchi hizo hasa ISIS.