Mar 24, 2016 08:27 UTC
  • Wanachama 400 wa Daesh wameingia Ulaya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi

Kundi la kigaidi la Daesh limetuma wanachama 400 katika nchi za Ulaya kwa ajili ya kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Maafisa usalama wa Ulaya wameripoti kuwa, kundi la kigaidi la Daesh limewapa mafunzo wanachama wasiopungua 400 kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Ulaya. Maafisa usalama wa Iraq na nchi za Ulaya wamesema kundi hilo limeanzisha kambi za kutoa mafunzo maalumu ya jinsi ya kufanya mashambulizi katika nchi za Magharibi.

Maafisa hao wanasisitiza kuwa, wapiganaji hao wameamriwa kutafuta mbinu na wakati mwafaka kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi hayo.

Jumanne iliyopita wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh walifanya mashambulizi matatu katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brassels ambao pia ni makao makuu ya Umoja wa Ulaya na kuua watu wasiopungua 31. Watu wengine 270 walijeruhiwa katika hujuma hiyo iliyolenga uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni ya chini kwa chini. Mashambulizi hayo yamezua hofu kubwa katika nchi nyingine za Ulaya.

Tags