Tillerson: Niko tayari kufanya mazungumzo na Korea ya Kaskazini
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37543-tillerson_niko_tayari_kufanya_mazungumzo_na_korea_ya_kaskazini
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ametangaza kuwa Washington ina hamu ya kufanya mazungumzo na Pyong Yang bila ya sharti lolote kuhusu kuipokonya silaha Korea ya Kaskazini.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 13, 2017 07:54 UTC
  • Tillerson: Niko tayari kufanya mazungumzo na Korea ya Kaskazini

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ametangaza kuwa Washington ina hamu ya kufanya mazungumzo na Pyong Yang bila ya sharti lolote kuhusu kuipokonya silaha Korea ya Kaskazini.

Akizungumza jana katika Baraza la Antlantic mjini Washington, Rex Tillerson aliitaja Korea ya Kaskazini kuwa ni tishio kuu kwa dunia na Marekani na kudai kuwa tishio hilo la Korea ya Kaskazini limekuwa kubwa kiasi kwamba haliwezi kupuuzwa zaidi ya hapo. 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani ameongeza kuwa nchi hiyo ina mpango wa kuhitimisha uvumilivu wa kistratejia. Tillerson amesisitiza kuwa siasa za Washington kuhusu Korea ya Kaskazini ziko wazi kikamilifu na ametaka Peninsula ya Korea iwe sehemu isiyokuwa na silaha zozote za nyuklia. Mivutano katika Peninsula ya Korea imeshika kasi kufuatia matamshi ya vitisho ya Rais Donadl Trump wa Marekani ya kutaka kuanzisha vita dhidi ya Korea ya Kaskazini. Trump ametishia mara kadhaa kuishambulia kijeshi nchi hiyo. 

Washington imekuwa ikitaka kusitishwa majaribio ya kijeshi na nyuklia ya Korea ya Kaskazini, hata hivyo Pyong Yang imesisitiza mara kadhaa kwamba itaendelea kuimarisha uwezo wake wa kijeshi na wa kushambulia adui madhali Marekani na nchi waitifaki wake zingali zinaendelea kutoa vitisho dhidi yake.   

Moja ya jaribio la kombora lililofanywa na Korea ya Kaskazini