Trump asema Marekani ilitumia kiujinga $Trilioni 7 Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37979-trump_asema_marekani_ilitumia_kiujinga_trilioni_7_mashariki_ya_kati
Baada ya kupata pigo katika Umoja wa Mataifa, Rais Donald Trump wa Marekani sasa amesema Marekani imetumia kijinga dola trillioni saba Mashariki ya Kati
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Dec 23, 2017 11:47 UTC
  • Trump asema Marekani ilitumia kiujinga $Trilioni 7 Mashariki ya Kati

Baada ya kupata pigo katika Umoja wa Mataifa, Rais Donald Trump wa Marekani sasa amesema Marekani imetumia kijinga dola trillioni saba Mashariki ya Kati

Katika ujumbe wake kupitia mtandano wa kijamii wa twitter, Trump amesema, "Natabiri kuwa tutaanza kushirikiana na Wademocrat na tuanze kujenga upya miundo msingi ya nchi. Baada ya kutumia kijinga dola trilioni 7 Mashariki ya Kati, sasa ni wakati wa kuijenga upya nchi yetu!

Ujumbe huo wa Twitter umekuja baada ya Trump kushindwa na kudhalilika katika Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa ambalo limepiga kura ya kuunga mkono azimio ambalo liliitaka Marekani ibatilishe uamuzi wake wa kuitambua Quds Tukufu (Jerusalem) kama mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kabla ya upigaji kuwa huo, Trump alikuwa ametisha kuwa, Marekani itakata misaada yakw kwa nchi ambazo zitapinga uamuzi huo kuhusu Quds katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kura zilivyopigwa katika kikao cha Baraza Kuu la UN kupinga uamuzi wa Trump kuhusu Quds Tukufu

Trump alilalamika kuwa nchi huchukua misaada ya mamilioni au hata mabilioni ya dola kutoka Marekani na kisha zinapiga kura dhidi ya Marekani. Amesema sasa Marekani haitatoa misaada kwa nchi hizo na hivyo itaokoa kiasi kikubwa cha fedha. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley pia kabla ya upigaji kura alitoa vitisho na kuzionya nchi ambazo zitapinga uamuzi huo wa Trump kuhusu Quds kuwa zitaadhibiwa.

Lakini nchi nyingi duniani zilipuuza vitisho hivyo vya Marekani ambapo katika kikao cha Baraza Kuu siku ya Alhamisi iliyopita nchi 128 zilipiga kura ya kupinga uamuzi huo wa Trump kuhusu Quds huku nchi tisa tu zikiunga mkono uamuzi huo na zingine 35 zikijizuia kupiga kura na nchi zingine 21 hazikushiriki katika kikao hicho. Misri ambayo ni kati ya nchi zinazopata misaada mikubwa ya kijeshi kutoka Marekani ndio iliyowasilisha rasimu ya azimio hilo la kupinga uamuzi wa Trump.

Sasa Trump anaonekana kutaka kubadilisha fedheha hiyo kuwa fursa kwa kusema badala ya kutoa misaada ya kigeni atajishughulisha na kukarabati miundo msingi ya Marekani iliyochakaa.