Jan 15, 2018 07:37 UTC
  • Watu 43 wauawa katika ufyatulianaji risasi Marekani

Watu wasipoungua 43 wameuawa katika kipindi cha masaa 24 nchini Marekani katika matukio ya ufyatulianaji risasi nchini humo.

Kwa mujibu wa takwimu za Mashambulio ya Bunduki nchini Marekani, watu hao wameuawa katika majimbo ya Texas,Missouri, Minnesota, Florida, Illinois na Alabama

Takwimu zinaonyesha kuwa katika vitendo 110 vya ufatulianaji risasi kati ya Ijumaa na Jumamosi, watu 43 waliuawa na wengine 64 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa Kituo cha Takwimu za Mashambulio ya Bunduki Marekani mwaka 2017, kulikuwa na matukio 61,000  ya ufyatulianaji risasi kiholela nchini humo.

Afisa wa polisi akikabiliana na uhalifu mtaani nchini Marekani

Aidha kituo hicho kinasema kati ya Januari mwaka 2016 hadi Disemba 29 mwaka huo,  jumla ya matukio 57,371 ya ufyatuaji risasi yaliripotiwa katika maeneo mbalimbali ya Marekani ambayo yalisababisha watu 14,859 kuuawa na wengine 30,315 kujeruhiwa.

Tags