Waigizaji maarufu wa Bollywood waliomsusa Netanyahu India, wazidi kupongezwa duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i39405-waigizaji_maarufu_wa_bollywood_waliomsusa_netanyahu_india_wazidi_kupongezwa_duniani
Duru mbalimbali duniani, zimeendelea kuwapongeza wacheza filamu mashuhuri watatu wa Tasnia ya Filamu ya India 'Bollywood' kwa hatua yao ya kususa kuonana na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel wakati alipotembelea India hivi karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 24, 2018 01:23 UTC
  • Waigizaji maarufu wa Bollywood waliomsusa Netanyahu India, wazidi kupongezwa duniani

Duru mbalimbali duniani, zimeendelea kuwapongeza wacheza filamu mashuhuri watatu wa Tasnia ya Filamu ya India 'Bollywood' kwa hatua yao ya kususa kuonana na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel wakati alipotembelea India hivi karibuni.

Wachezafilamu hao ambao ni Shah Rukh Khan, Salman Khan na Amir Khan, walisusia mkutano uliokuwa umeandaliwa kati ya Netanyahu na waigizaji filamu wa nchi hiyo. Ingawa hawajatoa maelezo yoyote juu ya sababu yao ya kumsusia Netanyahu, lakini vyombo mbalimbali vya habari duniani likiwemo pia gazeti la kila siku la Millî Gazete la nchini Uturuki, vimetangaza kuwa chanzo cha wachezafilamu hao kususa kukutana na waziri mkuu huyo wa Israel ni kupinga jinai zinazofanywa na utawala khabiti wa Israel dhidi ya raia madhlum wa Palestina.

Mita Bachchan kushoto alipopiga picha na Netanyahu, anayeua watoto wa Palestina

Katika uwanja huo, waigizaji na shakhsia mbalimbali nchini India wamekosoa vikali kitendo cha baadhi ya wachezafilamu wengine waliohudhuria mkutano huo, huku wakimshambulia zaidi Amitabh Bachchan kwa kitendo chake cha kupiga picha pamoja wa Netanyahu. Wakikosoa kitendo hicho, wamesema kuwa, ni jambo la kushangaza kwa mtu kama Bachchan kupiga picha na kiongozi huyo wa Israel ambaye mikono yake imetapakaa damu za raia madhlum wa Palestina. Miongoni mwa waliomshambulia vikali Bachchan ni mcheza filamu mashuhuri wa India Ajaz Khan, ambaye amemshambulia kupitia mtandao wa kijamii wa Youtube huku akimkumbusha jinai zinazofanywa na Israel kila uchao dhidi ya Wapalestina.

Ajaz Khan, mcheza filamu mashuhuri wa India kati ya waliomshambulia vikali Bachchan 

Aidha Ajaz Khan amesema kuwa, suala la kuisusa Israel na viongozi wake sio suala la kiimani, bali ni suala la kibinaadamu zaidi ambalo linamgusa mwanadamu yeyote duniani. Benjamin Netanyahu, aliwasili India wiki iliyopita kupitia mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Narendra Modi mjini New Delhi. Kabla na baada ya kuwasili India, maelfu ya raia wa nchi hiyo walifanya maandamano mtawalia wakilaani mahusiano kati ya New Delhi na Tel Aviv kutokana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na Israel kuwalenga Wapalestina.