Ripoti: Maelfu ya Wamarekani wanaishi katika utumwa mamboleo
Matokeo ya uchunguzi wa kimataifa uliofanyika nchini Marekani yameonesha kuwa, Maelfu ya raia wa nchi hiyo wanaishi katika hali mbaya iliyopewa jina la "utumwa mamboleo".
Matokeo ya uchunguzi uliofanywa na taasisi ya Walk Free Foundation yanasema kuwa zaidi ya Wamarekani laki nne wanaishi katika utumwa mamboleo.
Ripoti ya taasisi hiyo imesema watu 403,000 nchini Marekani wanaishi katika utumwa, ambao unajumuisha kufanya kazi ya kulazimika, utumwa wa ngono na ndoa ya kulazimishwa.
Mwasisi wa Walk Free Foundation, Andrew Forrest amesema kuwa Marekani inazidisha tatizo la utumwa kimataifa kwa kuagiza na kununua bidhaa ambazo zinazalishwa kwa kutumia wafanyakazi wa kulazimishwa.
Ripoti hiyyo imetolewa baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa, Wamarekani wasiopungua miliono 40 wanaishi katika hali ya umaskini. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ambayo imekabiliwa na maneno makali ya maafisa wa serikali ya Marekani, imesema raia milioni 18 na laki tano wa nchi hiyo manaishi katika ukata wa kupindukia.