Hotuba ya Mike Pompeo dhidi ya Iran yazomewa
Matamshi mabaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, yamekabiliwa na ukosolewaji mkali.
Inaelezwa kwamba idadi kubwa ya watu waliokuwa katika maktaba ya 'Ronald Reagan Presidential Library' wamepiga mayowe katika kujaribu kumzuia Pompeo kuendelea kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Iran. Kufuatia hali hiyo maafisa usalama wamelazimika kutumia nguvu kuwaondoa watu hao katika maktaba hiyo. Dakika chache baadaye na kufuatia kuendelea fujo, hatimaye hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ililazimika kusitishwa.
Katika hotuba ya leo aliyoitoa katika jimbo la California, Mike Pompeo alikariri tena tuhuma na uongo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Bila ya kuzingatia matamshi ya Trump, kwamba Marekani imetumia kiasi cha Dola trilioni saba katika vita vya Syria, Pompeo ameituhumu Iran kwamba inaiunga mkono makundi ya kigaidi.