China yaionya tena Marekani, yasema haitaipigia magoti Washington
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47078-china_yaionya_tena_marekani_yasema_haitaipigia_magoti_washington
Wizara ya Biashara ya China imetoa taarifa ambayo sambamba na kuwaonya viongozi wa Marekani imesema kuwa, nchi hiyo haitaipigia magoti Marekani katika vita vya kibiashara.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 28, 2018 07:02 UTC
  • China yaionya tena Marekani, yasema haitaipigia magoti Washington

Wizara ya Biashara ya China imetoa taarifa ambayo sambamba na kuwaonya viongozi wa Marekani imesema kuwa, nchi hiyo haitaipigia magoti Marekani katika vita vya kibiashara.

Taarifa hiyo iliyotolewa Jumamosi ya leo imeashiria ukosoaji wa Rais Donald Trump, Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya China unaosababishwa na chuki aliyonayo kwa nchi hiyo na kadhalika sera zake za kutumia mabavu na kupenda makuu za Washington na kusisitiza kwamba, mienendo hiyo haitakuwa na taathira yoyote kwa China.

Ripoti hiyo imeongeza kwamba, Marekani inakusudia kuvuruga muundo wa kiuchumi uliopo na kukanyaga sheria za Shirika la Biashara Duniani (WTO) na hivyo kupelekea kuibuka makundi na mpasuko wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za dunia. Taarifa imetolewa katika hali ambayo katika siku zijazo Marekani inakusudia kuzidisha ushuru wa forodha wa Dola bilioni 16 kwa bidhaa za China zinazoingizwa nchini humo.

Gao Feng, Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China

Kabla ya hapo pia Washington iliipandishia China ushuru wa forodha wa dola bilioni 34.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China, Gao Feng amekosoa mwenendo wa Shirika la Biashara Duniani katika vita vya kibiashara vya Marekani na kusema kuwa hali ya sasa inalazimu kufanyiwa marekebisho shirika hilo na kwamba Beijing inaunga mkono marekebisho hayo. Vita vya kibiashara kati ya Marekani na China vilianza tarehe 8 Machi mwaka huu, kufuatia uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuzidisha ushuru wa forodha kwa bidhaa za China zinazoingizwa nchini humo.