Afisa wa UN: Trump anairejesha dunia kipindi cha karne za kati
Afisa mmoja wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani anaielekeza dunia katika zama za udhibiti wa nguvu na mabavu dhidi ya sheria na kuirejesha katika zama za karne za kati.
Mkuu wa jumuiya ya Mpango ya Ustawi ya Umoja wa Mataifa, Achim Steiner amekosoa vikali sera na siasa za Donald Trump na kusema: Kuna hitilafu zinazowazuia washika kufikia makubaliano na Marekani kuhusu masuala mbalimbali kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na biashara ya kimataifa.
Steiner amesema kuwa, kwa mwenendo wa sasa nchi za Magharibi zitapoteza uwezo na ushawishi wao.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameashiria misimamo ya Trump katika mikutano kadhaa iliyofanyika wiki za hivi karibuni kama mkutano wa wanachama wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) na mkutano wa viongozi wa G7 na kusema ulimwengu wa sasa wa Magharibi unaoongozwa na Marekani haufanani tena ule wa miaka ya nyuma kutokana na matukio ya hivi karibuni.
Sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja na zinazokiuka sheria za Rais wa sasa wa Marekani zimezusha mivutano na hitilafu kubwa katika masuala mengi ya kimataifa.