India: Hatutoacha kununua mafuta ya Iran licha ya Marekani kututaka tuache
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47786-india_hatutoacha_kununua_mafuta_ya_iran_licha_ya_marekani_kututaka_tuache
Afisa mmoja wa ngazi ya juu nchini India amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo itaendelea kununua mafuta ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 30, 2018 11:24 UTC
  • India: Hatutoacha kununua mafuta ya Iran licha ya Marekani kututaka tuache

Afisa mmoja wa ngazi ya juu nchini India amesema kuwa, serikali ya nchi hiyo itaendelea kununua mafuta ya Iran.

Afisa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake amesisitiza kwamba, nchi yake haitasimamisha ununuzi wa mafuta ya Iran na kwamba katika safari ijayo nchini Marekani, viongozi wa India wataieleza Washington stratijia ya mwisho kuhusiana na ununuzi wa mafuta hayo. Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Sushma Swaraj pamoja na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Nirmala Sitharaman wamepanga kufanya safari nchini Marekani mwezi ujao wa Septemba kwa ajili ya kushiriki kikao cha 2+2 pamoja na viongozi wa Marekani. India inatarajia kwamba baada ya kukutana na viongozi wa ngazi ya juu wa Marekani, kutawekwa wazi suala la ununuzi wa mafuta ya Iran.

Njama za Trump za kuzuia uuzwaji mafuta ya Iran zinaendelea kugonga mwamba

Tarehe 8 mwezi Mei mwaka huu, Marekani ilijiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran na kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuzuia uuzaji mafuta wa nchi hii hadi kufikia sifuri kuanzia tarehe nne Novemba mwaka huu. Suala hilo lilipingwa na nchi nyingi wanunuzi wa mafuta ya Iran ikiwemo India. Tangu Rais Donald Trump alipoingia katika ikulu ya White House, amekuwa akitekeleza siasa za uhasama, dhidi ya Jamhuiri ya Kiislamu ya Iran.