Apr 11, 2016 07:23 UTC
  • US: Kerry hatawaomba msahamaha Wajapan kutokana na mauaji ya Hiroshima

Marekani imesema Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo hataliomba msamaha taifa la Japan kutokana na mauaji ya maelfu ya watu wa Hiroshima yaliyofanywa na ndege za Marekani mwaka 1945.

Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Washington ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema hakuna mpango wowote wa John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye aliwasili mjini Hiroshima jana Jumapili kuwaomba radhi wananchi wa Japan kutokana na ukatili uliofanywa na serikali ya Washington katika Vita vya Pili vya Dunia. Imearifiwa kuwa, Kerry yuko nchini Japan kuandaa mazingira ya safari ya Rais Barack Obama wa Marekani nchini humo mwezi ujao wa Mei na kuhudhuria kongamano la Kundi la G7. Itakumbukwa kuwa, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia ndege za kivita za Marekani zilifanya mashambulizi makubwa dhidi ya mji mkuu wa Japan, Tokyo. Karibu raia laki moja wa nchi hiyo waliuawa katika mashambulizi hayo.

Hata hivyo Japan haikusalimu amri hadi Mwezi Agosti mwaka huo huo wa 1945 wakati Marekani iliposhambulia kwa mabomu ya atomiki miji ya Hiroshima na Nagasaki na kuua maelfu ya raia wasio na hatia.

Watu laki 1 na elfu 40 waliuawa mjini Hiroshima na wengine 70 elfu waliuawa Nagasaki. 

Tags