India yaamua kuwafukuza wakimbizi Waislamu wa Rohingya
Waziri wa Mambo ya Ndani wa India amesema kuwa serikali ya New Delhi imeamua kuwaondoa wakimbizi Waislamu wa Rohingya waliokimbilia nchini humo.
Rajnath Singh, sambamba na kudai kuwa uwepo wa wakimbizi hao Waislamu nchini India si halali amezitaka tawala za majimbo yote ya nchi hiyo kutoa taarifa za wakimbizi hao kwa ajili ya kuwaondoa India na kuwarejesha nchini kwao Myanmar. Waziri wa Mambo ya Ndani wa India ameongeza kuwa, Waislamu wote wa Rohingya nchini India ni wahajiri haramu na hawatakiwi kujaribu kuwa na nyaraka zinazowaonyesha kwamba ni raia wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, wakimbizi Waislamu wa Rohingya nchini India ni elfu 40.
Uamuzi wa serikali ya New Delhi wa kuwaondoa Waislamu hao wa Rohingya kwa madai kuwa ni wahajiri haramu na kuwarejesha nchini Myanmar, umechukuliwa katika hali ambayo Mabudha wenye misimamo mikali wa nchi hiyo nao wanawataja Waislamu hao wa Rohingya kuwa ni wahajiri haramu ndani ya nchi yao ya asili yaani Myanmar.
Mabudha hao magaidi kwa kushirikiana na askari wa serikali ya Myanmar wanawanyanyasa vibaya Waislamu wa jamii ya Rohingya na wamekuwa wakifanya mauaji na jinai kubwa dhidi ya Waislamu hao. Mashambulizi yaliyozuka tarehe 25 Agosti mwaka jana ambapo askari na Mabudha hao waliwalenga Waislamu wa Rohingya ndani ya jimbo la Rakhine, yamepelekea zaidi ya Waislamu elfu sita kuuawa na wengine karibu milioni moja kuwa wakimbizi ndani na nje ya Myanmar.