Bei ya nyumba yapanda zaidi Marekani, huku uwezo wa kununua ukishuka
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48506-bei_ya_nyumba_yapanda_zaidi_marekani_huku_uwezo_wa_kununua_ukishuka
Licha ya madai ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuboreka hali ya kiuchumi nchini humo, gazeti la New York Times limeandika habari ya ongezeko la bei ya nyumba na kupungua uwezo wa kununua makazi kwa raia wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 01, 2018 04:50 UTC
  • Bei ya nyumba yapanda zaidi Marekani, huku uwezo wa kununua ukishuka

Licha ya madai ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuboreka hali ya kiuchumi nchini humo, gazeti la New York Times limeandika habari ya ongezeko la bei ya nyumba na kupungua uwezo wa kununua makazi kwa raia wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, kiwango cha ununuzi wa nyumba na shughuli za ujenzi katika miezi ya hivi karibuni kimeendelea kupungua kati ya Wamarekani. Aidha nyumba za kuishi zimeendelea kusalia wazi ambapo wauzaji wamelazimika kutumia njia mpya za matangazo kwa ajili ya kuwavutia wanunuzi. Gazeti la New York Times limeongeza kwamba, miji mingi kama vile New York, Seattle na hata San Francisco ambako soko la nyumba lilikuwa na ustawi hadi sasa linashuhudia mkwamo mkubwa. Kwa mujibu wa habari hiyo, wataalamu na wanaharakati wa sekta ya makazi nchini Marekani wanaamini ongezeko la bei ya makazi na kupungua kwa uwezo wa kununua kwa wahitaji wa makazi hayo limeshika kasi katika pembe zote za nchi hiyo.

Rais Donald Trump ambaye anadai kuboresha uchumi wa Marekani

Kuhusiana na suala hilo, Steve Dani Liu, mtaalamu wa sekta ya makazi ameliambia gazeti la New York Times kwamba, suala la hali mbaya ya makazi, kuendelea kupungua mishahara ya wafanyakazi na kupungua uwezo wa kununua ni mambo yanayoendelea kushuhudiwa kila siku nchini humo. Kufuatia hali hiyo wataalamu wa mambo wameionya serikali ya Rais Donald Trump ambaye hivi karibuni, akihutubia mkutano wa 73 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa alidai kuwa uchumi wa Marekani umestawi na kupungua kiwango cha ukosefu wa ajira.