Trump apatwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuuzuliwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50634-trump_apatwa_na_wasiwasi_kuhusu_uwezekano_wa_kuuzuliwa
Rais wa Marekani ameonyesha radiamali yake kufuatia kuenea habari kuhusu uamuzi wa Wademocrats katika kongresi ya nchi hiyo wa kutaka kumsaili kwa lengo la kumuuzulu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 04, 2019 13:03 UTC
  • Trump apatwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuuzuliwa

Rais wa Marekani ameonyesha radiamali yake kufuatia kuenea habari kuhusu uamuzi wa Wademocrats katika kongresi ya nchi hiyo wa kutaka kumsaili kwa lengo la kumuuzulu.

Leo Ijumaa Rais Trump ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa twitter akiwaeleza hivi Wademokcats na hapa ninamnukuu "Hao wanataka kunisaili kwa sababu tu wanajua kwamba hawawezi kushinda katika uchaguzi wa 2020; mini nina nafasi kubwa zaidi" mwisho wa kunukuu.  

Trump aidha ameandika kuwa: "Masoko ya fedha duniani yatavurugika iwapo nitasailiwa." Baada ya Wademocrats kudhibiti kongresi ya Marekani, moja ya hatua ambazo kuna uwezekano mkubwa zikachukuliwa dhidi ya Trump ni kumsaili kwa lengo la kumuuzulu. Kuhusiana na suala hilo, duru moja ya kuaminika imeiambia televisheni ya CNN kuwa Trump ameeleza kutiwa wasiwasi na kuwepo uwezekano wa wawakilishi wa chama cha Democrat katika bunge la nchi hiyo kutaka asailiwe. 

Wakati huo huo duru nyingine ndani ya ikulu ya Marekani (White House)  imeiambia CNN kwamba, wasaidizi wa Trump wanaamini kuwa suala pekee linaloweza kupelekea kuanza mchakato huo wa kumsaili Trump ni ukiukaji sheria wa masuala ya kifedha uliofanywa na aliyekuwa wakili wake binafsi Michael Cohen na hatua ya wakili huyo ya kuwalipa pesa wanawake ambao Trump alikuwa na uhusiano nao wa kingono.  

Michael Cohen, Wakili binafsi wa Rais Donald Trump