Mkurugenzi wa HRW: Misimamo ya Marekani kuhusu haki za binadamu inagongana
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51460-mkurugenzi_wa_hrw_misimamo_ya_marekani_kuhusu_haki_za_binadamu_inagongana
Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za bindamu la Human Rights Watch amesema mienendo ya serikali Marekani kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu inagongana na kukinzana.
(last modified 2026-08-08T07:03:00+00:00 )
Feb 10, 2019 09:26 UTC
  • Mkurugenzi wa HRW: Misimamo ya Marekani kuhusu haki za binadamu inagongana

Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za bindamu la Human Rights Watch amesema mienendo ya serikali Marekani kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu inagongana na kukinzana.

Kenneth Roth amesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter kwamba: Marekani inanyamazia kimya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na washirika wake kama Saudi Arabia na utawala wa Israel.

Ripoti zinasema tangu baada kufuchuliwa fedheha ya kuuliwa kinyama mwandishi na mkosoaji wa serikali ya SaudiA Arabia, Jamal Khashoggi na mauaji yanayofanwya na Saudi Arabia dhidi ya raia wasio na hatia nchini Yemen, Marekani imekuwa chini ya mashinikizo makubwa ya kimataifa yanayoitaka ibadili mienendo yake kuhusu utawala wa kifalme wa Saudia. Hata hivyo serikali ya Donald Trump imeendelea kuukingia kifua utawala huo unaoendela kukiuka haki za binadamu hususan haki za Waislamu wa madhehebu ya Shia na wanaharakati wa masuala ya kijamii.

Jinai za Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya raia wa Yemen wasio na hatia

Marekani pia imezidisha himaya na misaada yake kwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaoua na kukiuka haki za raia wasio na hatia wa Palestina hususan wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

Utawala huo wa Kizayuni umekuwa ukikosolewa sana na jumuiya mbalimbali za kimataifa za kutetea haki za binadamu kutokana na mauaji ya raia wa Palestina hususan raia wanaoshiriki katika maandamano ya amani ya Haki ya Kurejea katika eneo la Ukanda wa Gaza.