Trump: Ni kweli vitendo vya ukatili vimeongezeka nchini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51557-trump_ni_kweli_vitendo_vya_ukatili_vimeongezeka_nchini_marekani
Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kwamba jinai za ukatili nchini humo zimeongezeka maradufu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 14, 2019 23:20 UTC
  • Trump: Ni kweli vitendo vya ukatili vimeongezeka nchini Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani amekiri kwamba jinai za ukatili nchini humo zimeongezeka maradufu.

Trump ameyasema hayo katika kikao cha maafisa wa polisi wa Marekani na kusema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita tangu alipoapishwa kuwa rais wa Marekani hadi sasa jinai za vitendo vya utumiaji mabavu na ukatili vimeongezeka kwa asilimia 8 huku kiwango cha mauaji nacho kikiongezeka kwa asilimia 20. Aidha Trump amedai kwamba kupunguza jinai hizo, ni katika vipaumbele vikuu vya serikali yake. Inafaa kuashiria kuwa, Marekani inakabiliwa na wimbi la vitendo vya ukatili, mauaji, utekaji nyara watu na mashambulizi ya utumiaji silaha. Kwa mwaka maelfu ya watu huuawa na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti rasmi, karibu silaha za moto milioni 270 hadi 300 zimetapakaa kati ya raia wa nchi hiyo, hii ikiwa na maana kwamba karibu kila Mmarekani mmoja anamiliki silaha moto.

Trump anaunga mkono magenge ya wauzaji na wamiliki wa silaha moto nchini Marekani

Licha ya makundi mbalimbali ya kutetea haki za kiraia nchini humo kushinikiza kuwekwa sheria kali zinazozuia uuzaji holela wa silaha moto nchini humo, lakini hadi sasa serikali ya Washington imeshindwa kuweka sheria hiyo kutokana na satua kubwa ya lobi ya magenge yanayouza silaha hizo. Inafaa kuashiria kuwa, Rais Donald Trump ni miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa umiliki wa silaha moto nchini humo ambapo tangu baada ya kuingia madarakani alitangaza wazi kwamba baada ya miaka 8 ya kukandamizwa haki zao, wamiliki wa silaha hizo, sasa wamepata muungaji mkono wao wa kweli katika ikulu ya White House.