Mogherini: EU haitatilia maanani uamuzi wa Uingereza dhidi ya Hizbullah
Mkuu wa Sera za Kigeni katika Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema umoja huo hautatilia maanani hatua ya Uingereza kuiwekea vikwazo Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Youm Al-Sabie, Mogherini amesema uamuzi wa Uingereza wa kuwekea vikwazo matawi yote ya Hizbullah ni kuitaja harakati hiyo kuwa 'kundi la kigaidi' ni uamuzi wa ndani ya nchi na wala hauathiri maamuzi ya Umoja wa Ulaya.
Akizungumza na waandishi habari akiwa ameandamana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Gebran Bassil mjini Beirtu amesema: "Umoja wa Ulaya utaunga mkono Lebanon katika kukabiliana na matatizo na changamoto zilizopo."
Serikali ya Uingereza siku ya Jumatatu ilitioa madai dhidi ya Harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kuitangaza kuwa eti ni tishio kwa usalama na kwa msingi huo ikaiweka katika orodha ya makundi ya kigaidi.
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekosoa uamuzi huo wa Uingereza na kusema hakuna nchi yoyote yenye haki ya kukiweka katika orodha ya makundi ya kigaidi chama cha kisiasa cha Lebanon ambacho kina mawaziri katika serikali ya Lebanon.
Macron ameendelea kusema kuwa, serikali ya Ufaransa ina maingiliano na tawi la kisiasa la Hizbullah ambalo liko katika serikali ya Lebanon.
Kama ilivyotarajiwa, Marekani imeunga mkono uamuzi huo wa Uingereza.