Uturuki: Hatujaakhirisha uamuzi wa kununua ngao ya S 400 ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53844-uturuki_hatujaakhirisha_uamuzi_wa_kununua_ngao_ya_s_400_ya_russia
Serikli ya Uturuki imekadhibisha habari zilizoenezwa kwamba imesimamisha kwa muda mchakato wa ununuzi wa ngao ya makombora ya S 400 ya Russia kwa pendekezo la Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 01, 2019 03:04 UTC
  • Uturuki: Hatujaakhirisha uamuzi wa kununua ngao ya S 400 ya Russia

Serikli ya Uturuki imekadhibisha habari zilizoenezwa kwamba imesimamisha kwa muda mchakato wa ununuzi wa ngao ya makombora ya S 400 ya Russia kwa pendekezo la Marekani.

Hami Aksoy, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki sambamba na kukadhibisha habari hiyo amesisitiza kwamba, mchakato wa ununuzi wa ngao hiyo ya makombora ya S 400 unaendelea kama ulivyopangwa na wala hakuna suala la kuahirishwa kwake. Aksoy amebainisha kwamba pendekezo la Uturuki kwa ajili ya kuundwa jopo kazi na viongozi wa Marekani kuhusiana na kadhia ya ununuzi wa ngao hiyo, ni habari isiyo na itibari. Kwa mara kadhaa serikali ya Washington imekuwa ikiitishia Uturuki kwamba inakusudia kuiwekea vikwazo vikali iwapo itanunua ngao ya makombora ya S 400 kutoka Russia.

Ngao ya makombora ya S 400 ya Russia

Kadhalika Marekani imeonya kwamba katika radiamali yake itakayoichukua kufuatia hatua hiyo ya Ankara itafuta uamuzi wa kuiuzia ndege za kivita aina ya F 35. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Uturuki wametangaza kwamba, mchakato wa mauzo ya silaha ya S 400 kutoka Russia utaanza msimu wa joto mwaka huu. Serikali ya Makarekani inadai kwamba ngao ya makombora ya S 400 ya Russia inaweza kudukua taarifa za Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO kwa manufaa ya Russia.