Marekani yashadidisha siasa zake dhidi ya wahajiri
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55527-marekani_yashadidisha_siasa_zake_dhidi_ya_wahajiri
Marekani imesema itaanza kutekeleza sheria mpya dhidi ya wahajiri na hivyo kuzidisha vigingi na vizuizi dhidi ya watoto na familia za wahajiri nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 22, 2019 02:37 UTC
  • Marekani yashadidisha siasa zake dhidi ya wahajiri

Marekani imesema itaanza kutekeleza sheria mpya dhidi ya wahajiri na hivyo kuzidisha vigingi na vizuizi dhidi ya watoto na familia za wahajiri nchini humo.

Serikali ya Marekani jana ilitangaza kuwa hatua ambazo zinaanza kutekelezwa zinaziruhusu taasisi za utekelezaji sheria kuwatia mbaroni kwa muda usiojulikana watoto wahajiri na familia zao. Serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani imeeleza kuwa, inachukua hatua ambazo zinavipatia mamlaka vyombo vya sheria vya nchi hiyo kuwatia mbaroni  watoto wa wahajiri bila ya waraka wowote wa kisheria. 

Sera hizo mpya ambazo zitaanza kutekelezwa katika siku 60 zijazo haziainishi kipindi malumu cha kutiwa mbaroni watoto hao wa wahajiri au familia zao.

Trump jana Jumatano alisema kuwa sheria hizo na ujenzi wa ukuta wa mpakani vitapunguza idadi ya wahajiri haramu wanaojaribu kuingia Marekani. Taasisi mbalimbali za kiraia ikiwemo Akademia ya Magonjwa ya Watoto ya Marekani (AAP) zimekuwa zikiitahadharisha serikali ya Trump kuhusu taathira mbaya za kimwili na kisaikolojia za kuwashikilia korokoroni watoto wahajiri.

Polisi wa Marekani wakiwatenganisha watoto wahajiri na familia zao
 

Wanaharakati wa kiraia na taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa pia mara kadhaa zimeeleza wasiwasi wao kuhusu kushtadi vizuizi na hatua za kuzibana familia za wahajiri na watoto wao huko Marekani.