Trump awatisha mashahidi wa faili la kusailiwa kwake
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57374-trump_awatisha_mashahidi_wa_faili_la_kusailiwa_kwake
Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuwafukuza kazi mashahidi ambao wanashirikiana na kongresi ya nchi hiyo katika faili la kusailiwa kwake
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 19, 2019 23:01 UTC
  • Trump awatisha mashahidi wa faili la kusailiwa kwake

Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kuwafukuza kazi mashahidi ambao wanashirikiana na kongresi ya nchi hiyo katika faili la kusailiwa kwake

Kwa mujibu wa habari hiyo, vitisho vya Trump vinawahusu watumishi wa vitengo tofauti vya serikali ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ikulu ya White House. Vikao vya wazi vya kutoa ushahidi watu waliokuwa na taarifa za mawasiliano na pia mawasiliano ya simu kati ya Ikulu ya White House na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine katika bunge la wawakilishi la Marekani, vilianza kusikilizwa wiki iliyopita na kufikia sasa vikao viwili vimefanyika katika uwanja huo. Katika kikao cha kwanza cha wazi cha kusikiliza ushahidi, William B. Taylor, Jr, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani nchini Ukraine pamoja na George P. Kent, Naibu Msaidizi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, walitoa ushahidi wao mbele ya kamati ya intelijensia ya bunge la wawakilishi.

Faili la kumsaili Trump ambalo linamtia kiwewe rais huyo wa Marekani

Aidha katika kikao cha pili na ambacho kilifanyika siku ya Ijumaa iliyopita, Marie Yovanovitch, balozi wa zamani wa Marekani nchini Ukraine alitoa ushahidi wake mbele ya kamati hiyo. Katika mazungumzo ya simu kati ya Rais Donald Trump na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine hapo tarehe 25 Julai mwaka huu, rais huyo wa Marekani alimtaka  mwenzake huyo wa Ukraine afanye uchunguzi wa ufisadi wa kifedha dhidi ya Joe Biden, mshindani wake mtarajiwa katika uchaguzi wa rais wa mwakani pamoja na Hunter Biden, mtoto wa kiume wa Joe Biden. Kufichuliwa mazungumzo hayo kuliwafanya Wademocrat katika bunge la wawakilishi kuanzisha uchunguzi wenye lengo la kumsaili Trump.