Baadhi ya Warepublican wazidisha juhudi za kumfukuza Trump kutoka White House
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62378-baadhi_ya_warepublican_wazidisha_juhudi_za_kumfukuza_trump_kutoka_white_house
Kundi la maafisa wa chama cha Republican wanaompinga Rais Donald Trump wa Marekani ambaye anatazamiwa kubeba bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao, limezidisha jitihada za kumuondoa kiongozi huyo katika Ikulu ya White House.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 23, 2020 21:53 UTC
  • Baadhi ya Warepublican wazidisha juhudi za kumfukuza Trump kutoka White House

Kundi la maafisa wa chama cha Republican wanaompinga Rais Donald Trump wa Marekani ambaye anatazamiwa kubeba bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao, limezidisha jitihada za kumuondoa kiongozi huyo katika Ikulu ya White House.

Ripoti zinasema kuwa, baadhi ya wanastatijia wakubwa wa chama tawala cha Republican hawaridhishwi hata kidogo na utendaji wa Rais Donald Trump na wanamtambua kuwa ni alama ya fedheha na aibu. 

Kundi hilo linaendesha kampeni kabambe katika mtandao wa kijamii wa Twitter kukabiliana na Donald Trump.

Kampeni dhidi ya Trump katika mtandao wa Twitter ambazo zinasimamiwa na makundi kadhaa likiwemo lile la Lincoln Project, zinafuatiliwa na mamilioni ya watu hususan katika miezi ya karibuni. 

Donald Trump

Kampeni hizo zinamtuhumu Donald Trump kuwa amezembea sana na kufeli katika kukabiliana na mgogoro wa maambukizi ya virusi vya corona vilivyoua maelfu ya watu nchini Marekani na vilevile usimamizi mbaya wa masuala ya nchi.

Kundi la Lincoln Project lilianzishwa mwaka jana kwa ajili ya kampeni dhidi ya Donald Trump na limepata wafuasi wengi sana katika jamii ya Marekani.

Trump amekuwa akiwataja wakosoaji wake kuwa ni waongo na watu waliofilisika. 

Matokeo ya uchunguzi wa maoni yaliyofanyika siku za karibuni yanaonyesha kuwa, mgombea urais wa chama cha Democratic, Joe Biden amemuacha mbali mpinzani wake, Donald Trump.

Uchaguzi wa rais wa Marekani utafanyika mwishoni mwa mwaka huu.