Dakta Fauci atishiwa kuuawa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62677-dakta_fauci_atishiwa_kuuawa
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Mzio na Magonjwa ya kuambukiza ya Marekani (NIAID) ametangaza kuwa yeye na familia wake wamekuwa wakipokea vitisho vya kuuliwa kutokana matamshi aliyoyatoa kuhusu maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 07, 2020 23:54 UTC
  • Dakta Fauci atishiwa kuuawa

Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Mzio na Magonjwa ya kuambukiza ya Marekani (NIAID) ametangaza kuwa yeye na familia wake wamekuwa wakipokea vitisho vya kuuliwa kutokana matamshi aliyoyatoa kuhusu maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Dakta Anthony Fauci amesema kuwa yeye na familia yake  wametumiwa vitisho vya kuuliwa na bughudha za mara kwa mara. Dakta Fauci amesema kuwa kwa msingi huo amesema yeye na familia yake wanahitaji ulinzi. 

Ukweli mwingi ulioelezwa na Dakta Fauci kuhusu maambukizi ya virusi vya corona huko Marekani ni kinyume na matakwa ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo na waungaji mkono wake wenye misimamo ya kuchupa mipaka.  

Kasi kubwa ya maambukizi ya corona nchini Marekani 

Mkurugenzi huyo wa Taasisi ya Taifa ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza ya Marekani Ijumaa iliyopita Julai 31 alilumbana na kukabiliana vikali na Jim Jordan mwakilishi wa jimbo la Ohio wa chama cha Republican katika Kamati ya Kongresi ya Marekani kuhusu jinsi ya kudhibiti virusi vya corona. 

Dakta Fauci alishiriki kwenye mjadala huo huku idadi ya watu walioaga dunia kwa corona katika majimbo yasiyopungua 18 huko Marekani ikitajwa kuongezeka mara mbili. 

Dakta Anthony Fauci amekuwa akikosolewa wahafidhina ambao siku zote wamekuwa wakimpinga wakitaka kufunguliwa kikamilifu shughuli za kiuchumi nchini humo huku nchi hiyo ikiendelea kusumbuliwa na maambukizi makubwa ya corona.