Trump azusha kioja kipya kwa kutaka Wamarekani wapige kura mara mbili
Rais wa Marekani ametoa matamshi ya kushangaza kwa kutaka wananchi wapige kura mara mbili katika uchaguzi wa urais ili kuufanyia majaribio mfumo wa upigaji kura kwa njia ya posta.
Trump amesema, Wamarekani wapige kura mara moja kwa njia ya posta kisha wakapige kura tena kwenye vituo vya upigaji kura.
Trump ameongeza kuwa, ikiwa upigaji kura utakuwa umefanyika kwa namna inayoelezwa, wananchi hao hawataweza kupiga kura tena katika vituo vya uchaguzi.
Rais huyo wa Marekani anawashajiisha raia wa nchi hiyo kupiga kura mara mbili wakati kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
Ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kufanyika uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2020 Trump amekuwa akiendelea kutoa kauli za kudhoofisha utaratibu wa kupiga kura kwa njia ya posta.
Wademokrati wanaunga mkono upigaji kura kwa njia hiyo, lakini Trump amekusudia kukwamisha mchakato wa upigaji kura kwa kutumia utaratibu huo.
Hofu ya rais huyo wa Marekani ni kwamba, upigaji kura kwa wingi kwa njia ya posta utapunguza uwezekano wa yeye kushinda katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais.
Uchaguzi wa rais wa Marekani utafanyika tarehe 3 Novemba huku chunguzi mbalimbali za maoni zikiwa zinaonyesha kuwa mgombea wa chama cha Democrat Joe Biden angali amemtangulia Trump kwa kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda katika uchaguzi huo.../