Makanisa ya Wamarekani weusi: Trump anaunga mkono ugaidi wa wazungu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i63449-makanisa_ya_wamarekani_weusi_trump_anaunga_mkono_ugaidi_wa_wazungu
Viongozi wa kanisa la Wamarekani wenye asili ya Afrika (AME) wamemtuhumu Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kuwa anaunga mkono ugaidi wa wazungu dhidi ya wasiokuwa wazungu katika propaganda zake za uchaguzi wa rais.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 15, 2020 22:46 UTC
  • Makanisa ya Wamarekani weusi: Trump anaunga mkono ugaidi wa wazungu

Viongozi wa kanisa la Wamarekani wenye asili ya Afrika (AME) wamemtuhumu Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kuwa anaunga mkono ugaidi wa wazungu dhidi ya wasiokuwa wazungu katika propaganda zake za uchaguzi wa rais.

Viongozi wa kanisa la Wamarekani weusi wametoa wito wa kufutwa kampeni zinazochochea ubaguzi wa rangi na kuitaka Serikali ya Federali ya nchi hiyo kukabiliana na hatua kama hizo na vitisho vyake.

Hivi karibuni timu ya kampeni za uchaguzi wa rais ya Donald Trump ilisambamba filamu iliyopewa jina la "Kutana na Wafuasi wa Joe Biden" ambayo imewataja Wamarekani weusi wanaokwenda kanisani kuwa ni wahuni wanaovunja sheria.

Kanisa la Waafrika wa Marekani (AME) limetoa taarifa likilaani kampeni hizo za Trump ambazo zinawahusisha wafuasi wake na votendo vya kikatili. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, filamu na kampeni kama hizo zinachochea ugaidi wa wazungu dhidi ya watu weusi na kuzidisha mshambulizi dhidi ya Wamarekani weusi na makanisa yao.

Magadi wazungu wafuasi wa Donald Trump

Taarifa hiyo pia imeitaka Wizara ya Sheria ya Marekani kuchunguza kampeni za uchaguzi za Donald Trump. 
Awali timu ya kampeni za uchaguzi wa rais ya Donad Trump ilikuwa iwataja watu wanaoandamana kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani kuwa ni wahuni hatari wa makundi ya mrengo wa kushoto.