UN: Hali imekuwa ya kutisha Marekani kutokana na uchochezi wa Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64039-un_hali_imekuwa_ya_kutisha_marekani_kutokana_na_uchochezi_wa_trump
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kutokana na uchochezi wa rais wa Marekani, Donald Trump, machafuko na ukatili unatokana na chuki na uadui umeongezeka mno nchini humo na sasa hivi umefikia kiwango cha hatari sana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 15, 2020 23:06 UTC
  • UN: Hali imekuwa ya kutisha Marekani kutokana na uchochezi wa Trump

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kutokana na uchochezi wa rais wa Marekani, Donald Trump, machafuko na ukatili unatokana na chuki na uadui umeongezeka mno nchini humo na sasa hivi umefikia kiwango cha hatari sana.

Mtandao wa Business Insider umewanukuu maafisa wa Umoja wa Mataifa wakisema katika ripoti yao kwamba, uhalifu na ukatili unaotokana na chuki dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Asia umefikia kiwango cha kutisha katika kona zote za Marekani ambapo moja ya sababu zake ni uungaji mkono wa rais wa nchi hiyo Donald Trump, kwa chuki na vitendo vya kibaguzi vya wahalifu.

Hayo yameelezwa na maripota maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya ubaguzi wa rangi na haki za wageni ndani ya Marekani wakisema kwamba zaidi ya matukio 1800 ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Asia yaliripotiwa nchini humo katika kipindi cha baina ya mwezi Machi hadi Mei 2020.

Trump anawaunga mkono makatili kama hawa wanaouwa watu kamahivi, kwa damu baridi mchana kweupe

 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, viongozi wa Marekani wanapuuza kabisa kuchukua hatua zinazotakiwa za kusaka, kudhibiti na kuzuia vitendo vya ubaruzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni suala ambalo limeyafanya magenge ya ubaguzi wa rangi yapate nguvu na yahisi kwamba yanaweza kufanya ukatili wa aina yoyote ile bila ya kufuatiliwa kisheria.

Uchunguzi wa huko nyuma nao unaonesha kuwa, kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya matusi na matamshi ya jeuri yanayotolewa na Trump na kuongezeka uhalifu unatokana na chuki, ubaguzi wa rangi na kuchukia wageni huko Marekani.