Trump kushiriki maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i64614-trump_kushiriki_maandamano_ya_kupinga_matokeo_ya_uchaguzi_marekani
Rais anayeondoka wa Marekani, Donald Trump amesema yumkini leo atajiunga na wafuasi wake katika maandamano ya mjini Washington, ya kupinga mchakato na matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2020 03:51 UTC
  • Trump kushiriki maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Marekani

Rais anayeondoka wa Marekani, Donald Trump amesema yumkini leo atajiunga na wafuasi wake katika maandamano ya mjini Washington, ya kupinga mchakato na matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita.

Katika ujumbe wa Twitter, Trump amesema anatiwa moyo na wimbi la maandamano yanayoshuhudiwa katika kona mbalimbali za nchi, kulalamikia matokeo ya uchaguzi huo, na kuongeza kwamba huenda leo Jumamosi ataungana na wafuasi wake watakaondamana katika mji mkuu, Washington DC.  

Bila kutoa ushahidi wowote, Trump katika ujumbe huo ameendelea kubwabwaja kuwa kuna uchakachuaji na udanganyifu mkubwa wa kura kwa maslahi ya mshindani wake, Joe Biden.

Trump na Joe Biden

Hii ni katika hali ambayo, uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni nchini humo uliofanywa na shirika la habari la Reuters na Taasisi ya Ipsos unaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wananchi hao wanaamini kwamba Trump anang'ang'ania madaraka bila sababu kwani ameshindwa katika uchaguzi huo wa Novemba 3.

Kadhalika taasisi zilizohusika na uendeshaji wa uchaguzi huo zimesema kuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuweko uchakachuaji au kupotea kura za uchaguzi huo.