Dec 04, 2020 12:04 UTC
  • Yamkini Misikiti 76 ikafungwa Ufaransa katika kampeni dhidi ya Waislamu

Serikali ya Ufaransa imetangaza mpango mkubwa na ambao haujawahi kushuhudiwa wa kufanya upekuzi katika misikiti ya nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Drmanin amesema mpango huo unalenga kukabiliana na kile alichokitaja kuwa ni ‘misimamo mikali ya kidini’ huku akisema misikiti 76 inashukiwa kueneza itikadi za ‘kujitenga’.

Darmanin alitangaza Alhamisi kuwa, katika siku chache zijazo, kutafanyika upekuzi katika maeneo hayo ya ibada na itafungwa iwapo itabainika kuhusika na uenezaji wa ‘misimamo mikali’.

Aidha amesema wahajiri 66 wanaoishi Ufaransa kinyume cha sheria wanashukiwa kuhusika katika ‘uenezaji misimamo mikali’.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

Mwezi uliopita,  ikiwa ni katika kuendeleza kampeni dhidi ya asasi za Kiislamu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darminian alitangaza mpango wa kupiga marufuku Taasisi ya Kupambana na Chuki Dhidi ya Uislamu au Islamophobia Ufaransa (CCIF).

Mwezi Oktoba, Drmanin alitangaza nia ya kupiga marufuku asasi kadhaa za Kiislamu zisizo za kiserikali nchini humo.

Hayo yanajiri wakati ambao, matamshi ya hivi karibuni ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwamba Uislamu uko kwenye mgogoro duniani kote na msimamo wake wa kuunga makono kitendo kiovu cha jarida la nchi hiyo la Charlie Hebdo cha kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW kimeughadhibisha Ulimwengu wa Kiislamu.

Tags