Walebanoni waandamana kuunga mkono operesheni ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i80998-walebanoni_waandamana_kuunga_mkono_operesheni_ya_kijeshi_ya_russia_nchini_ukraine
Wakazi wa mji mkuu wa Lebanon, Beirut wamefanya maandamano wakishirikiana na Warussia wanaoishi nchini humo wakiunga mkono operesheni ya Jeshi la Russia dhidi ya "mafashisti wa Ukraine".
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 04, 2022 04:34 UTC
  • Walebanoni waandamana kuunga mkono operesheni ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine

Wakazi wa mji mkuu wa Lebanon, Beirut wamefanya maandamano wakishirikiana na Warussia wanaoishi nchini humo wakiunga mkono operesheni ya Jeshi la Russia dhidi ya "mafashisti wa Ukraine".

Walebanoni walioshiriki katika maandamano hayo walikuwa wakipiga nara za kulaani harakati za Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) na jinsi serikali ya Marekani inavyowatumia vibaya watu wa Ukraine kwa ajili ya kutimiza sera zake za kibeberu.

Waandamanaji hao walishikilia mabango yenye maandishi "Tunaunga mkono kuangamizwa kwa wanazi na mafashisti" na "Russia itasimama peke yake dhidi ya unazi". Baadhi ya waandamanaji hao pia  walibeba picha za wahanga wa mwaka 2014 katika eneo la Donbass.

Balozi wa Russia nchini Lebanon, Alexander Rudakov, amewashukuru watu wa Lebanon kwa kuunga mkono matukio ya sasa ya Ukraine na himaya yao kwa Shirikisho la Russia.

Operesheni ya sasa ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine inasemekana kuwa ni jibu kwa misimamo ya uhasama na hatua za Marekani na NATO, pamoja na msimamo wa serikali ya Ukraine wa kutotoa jibu la kimantiki kwa wasiwasi wa usalama wa serikali ya Moscow.

Rais wa Russia, Vladimir Putin Alhamisi tarehe 24 Februari aliamuru operesheni maalumu ya kijeshi katika eneo la Donbas kujibu ombi la msaada wa kijeshi kutoka kwa viongozi wa jamhuri za Donetsk na Luhansk huko Mashariki mwa Ukraine.