Russia: Njia pekee kwa Uturuki ni kuomba radhi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i8128-russia_njia_pekee_kwa_uturuki_ni_kuomba_radhi
Msemaji wa Rais wa Russia amesema kuwa kuomba radhi ndio njia pekee iliyonayo Uturuki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2016 11:00 UTC
  • Russia: Njia pekee kwa Uturuki ni kuomba radhi

Msemaji wa Rais wa Russia amesema kuwa kuomba radhi ndio njia pekee iliyonayo Uturuki.

Dmitry Peskov, msemaji wa Ikulu ya Russia Kremlin amesema kuwa Ankara haina njia nyingine ghairi ya kuiomba radhi rasmi Russia kwa kitendo chake cha kuitungua ndege ya kijeshi ya nchi hiyo mwaka jana katika mpaka wa Syria na Uturuki, ili iweze kurejesha uhusiano wake na Moscow katika hali ya kawaida.

Msemaji wa Rais wa Russia ameongeza kuwa uhusiano kati ya Ankara na Moscow unaweza kuhuishwa iwapo Uturuki itaiomba radhi rasmi Russia na kufidia hasara ilizopata Moscow kwa kutunguliwa ndege yake ya kivita aina ya Sokhoi-24. Peskov amesema hakuna njia nyingine katika uwanja huo.

Matamshi hayo ya msemaji wa Rais wa Russia yanaonekana kuwa ni sisitizo la msimamo wa huko nyuma wa Russia kwa serikali mpya ya Uturuki inayoongozwa na Waziri Mkuu Binali Yildrim na vile vile ni jibu kwa matamshi ya hivi majuzi yaliyotolewa na Mevlut Cavusoghlo, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo juu ya uwezekano wa kuundwa kamati ya kufuatilia uhuishaji wa uhusiano kati ya Moscow na Ankara.