Apr 09, 2023 02:16 UTC
  • Marekani imekithirisha uwekaji wa silaha zake za nyuklia katika bara la Ulaya

Shirika la habari la Sputnik limetangaza kuwa Marekani imekithirisha uwekaji silaha zake za nyuklia barani Ulaya.

Kwa mujibu wa shirika hilo, mchakato wa kupelekwa silaha za nyuklia za Marekani katika nchi nyingi za Ulaya umeongezeka  tangu vilipoanza vita vya Ukraine.
 
Kwa mujibu wa ripoti na nyaraka zilizotolewa na taasisi na mashirika ya Ulaya, Marekani ina makumi ya vituo vya silaha za nyuklia katika bara la Ulaya, ambavyo vimewekwa kufuatana na mpango wa pamoja wa nyuklia wa Shirika la kijeshi la NATO, lakini mahali hasa zilipo silaha hizo na idadi yake kamili haijulikani.

Hivi sasa, silaha za nyuklia za Marekani zimewekwa katika nchi za Ubelgiji, Ujerumani, Italia, Uholanzi na Uturuki kama sehemu ya mpango wa pamoja wa nyuklia wa NATO. Silaha hizo za nyuklia zimewekwa tu katika nchi hizo tano wanachama wa NATO lakini mmiliki wake ni Washington.

 
Baada ya kuanza vita nchini Ukraine mnamo Februari 2022, zilitolewa ripoti za pendekezo la Warsaw la kupelekwa silaha za nyuklia za Marekani nchini Poland.
 
Pendekezo hilo la Poland la kushauri ardhi ya nchi hiyo ifanywe kituo cha kuwekea silaha za nyuklia ni mfano wa karibuni zaidi wa wasiwasi unaoongezeka kuhusu uwezekano wa kutumiwa silaha za nyuklia.../

 

Tags