Russia: Tupo tayari kufanya mazungumzo na Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/world-i9820-russia_tupo_tayari_kufanya_mazungumzo_na_uturuki
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa Moscow ipo tayari kufanya mazungumzo na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 23, 2016 22:37 UTC
  • Russia: Tupo tayari kufanya mazungumzo na Uturuki

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa Moscow ipo tayari kufanya mazungumzo na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia leo Alkhamisi imetangaza kuwa, Moscow ipo tayari kufanya mazungumzo na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, iwapo nchi hiyo itakubali mwaliko wa Russia wa kufanyika mazungumzo hhayo katika mji wa pwani wa Sochi.

Uhusiano wa Moscow na Ankara uliiingia dosari na kuibua mivutano kufuatia kutunguliwa ndege ya kivita ya Russia na jeshi la anga la Uturuki katika ardhi ya Syria. Uturuki kwa mara kadhaa ilionyesha hamu yake ya kutaka kufufua uhusiano baina yake na Russia, lakini viongozi wa Russia walisema kuwa Uturuki inapaswa kuiomba radhi Moscow kwanza na kuilipa fidia kwa kuitungua ndege yake kama sharti la kufufua uhusiano kati ya nchi mbili hizo.

Iwapo Uturuki itakubali mwaliko huo wa Russia, basi mazungumzo kati ya pande mbili hizi yatafanyika katika mji wa pwani wa Sochi pambizoni mwa kikao cha Uchumi cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Bahari Nyeusi.