Sep 06, 2023 02:41 UTC
  • Jumatano, Septemba 6, 2023

Leo ni Jumatano tarehe 20 Mfunguo Tano Safar 1445 Hijria sawa na Septemba 6 mwaka 2022 Milaadia.

Siku kama ya leo miaka 1384 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein bin Ali (as) na watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria.

Majlisi ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume na masahaba zake watiifu ambao walisabilia roho zao katika ardhi ya Karbala kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu.

Siku kama ya leo miaka 257 iliyopita, alizaliwa John Dalton, msomi na mtaalamu wa fizikia wa Kingereza katika familia ya watu wa kijijini.

Kutokana na Dalton kupendelea sana elimu na licha ya kukabiliwa na matatizo mengi, alifanikiwa kwenda shuleni na kujifunza mambo mbalimbali. Ni wakati huo ndipo alipoanza kufanya uchunguzi na utafiti katika masuala mbalimbali ya kielimu. Dalton alibuni na kuvumbua mambo mengi katika uwanja wa fizikia, kemia na sayansi asilia baada ya utafiti mkubwa. 

Msomi huyo hakuchoka na badala yake aliendeleza utafiti mkubwa katika uga atomu. John Dalton alifariki dunia mwaka 1944.

John Dalton

Siku kama ya leo miaka 130 iliyopita, alizaliwa Ayatullah al-Udhma Mar’ashi Najafi mmoja wa maulama wakubwa wa Kiislamu katika mji wa Najaf nchini Iraq.

Baba yake ni Sayyid Shamsuddin Mahmoud Mar’ashi aliyekuwa miongoni mwa wanazuoni na mafaqihi wakubwa katika zama zake. Baada ya kukamilisha masomo ya awali na ya Kiislamu huko Najaf, Mar’ashi Najafi alianza kuhudhuria darsa na masomo ya Usul kwa Agha Dhiyau Iraqi na Sheikh Ahmad Kashif al-Ghitaa.

Ayatullah Mar’ashi Najafi alipata daraja ya juu ya elimu yya Ij’tihad akiwa na umri wa miaka 27. *

Ayatullah al-Udhma Mar’ashi Najafi

Siku kama ya leo miaka 58 iliyopita, jeshi la India lilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Pakistan kufuatia machafuko ya zaidi ya mwezi mmoja katika mipaka ya nchi mbili hizo.

Hivyo vilikuwa vita vya pili vikubwa kuwahi kutokea kati ya nchi mbili hizo jirani kuhusiana na eneo la Kashmir. Vita hivyo vilidumu kwa takribani wiki tatu.

Pakistan na India zilikubaliana kusimamisha mapigano kufuatia upatanishi wa Urusi ya zamani. Viongozi wa nchi mbili hizo hatimaye waliafikiana kuanza mazungumzo tarehe 10 mwezi Juni mwaka 1966 huko Tashkent mji mkuu wa Uzbekistan nchini ya upatanishi wa Waziri Mkuu wa Urusi ya zamani.

Japokuwa azimio la Tashkent lilibainisha njia za kumaliza mgogoro wa eneo la Kashmir na namna ya kuboresha uhusiano kati ya New Delhi na Islamabad na pia kukaribishwa na nchi mbalimbali duniani, lakini lilishindwa kumaliza hitilafu kati ya India na Pakistan kuhusu umiliki wa eneo la Kashmir. 

Vita vya Kashmir

Katika siku kama ya leo miaka 55 iliyopita, nchi ya Kiafrika ya Eswatini (Swaziland zamani) ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza na kila inapowadia siku kama ya leo husherekewa nchini humo kwa anwani ya siku ya taifa.

Kuimarika ukoloni wa Ulaya huko kusini mwa Afrika kulisababisha pia Eswatini kukaliwa kwa mabavu na wakoloni wa Ulaya.

Hatimaye katika siku kama ya leo nchi hiyo ndogo ya kusini mwa Afrika ilipata uhuru. Eswatini ina ukubwa wa kilomita mraba 17364 na kijiografia iko kusini mwa bara la Afrika ikiwa inapakana na nchi za Msumbiji na Afrika Kusini.

Siku kama ya leo miaka 45 iliyopita, baada ya kupamba moto harakati za mapambano ya wananchi Waislamu wa Iran dhidi ya utawala wa kidikteta wa Shah, kulifanyika maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali kote nchini.

Kwa sababu hiyo utawala wa Shah uliokuwa umepatwa na wasiwasi mkubwa kutokana na harakati hizo za mapinduzi, uliamua kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote ile.

Wakati huo huo huo Imam Ruhullah Khomeini MA aliyekuwa uhamishoni huko Najaf nchini Iraq alitoa taarifa akiwataka wananchi wa Iran kudumisha harakati za mapambano. Katika sehemu moja ya taarifa yake kwa wananchi, Imam Khomeini aliyataja maandamano yanayofanywa kwa ajili ya kufikia malengo ya Kiislamu kuwa ni ibada.

 

Tags