Mar 01, 2024 02:28 UTC
  • Ijumaa, tarehe Mosi Machi, 2024

Leo ni Ijumaa tarehe 20 Sha'ban 1445 Hijria sawa na tarehe Mosi Machi mwaka 2024.

Katika siku kama ya leo miaka 1060 iliyopita alifariki dunia mwanahistoria na mtaalamu maarufu wa vitabu wa Kiislamu Ibnu Nadeem.

Ibnu Nadeem alipata umaarufu kutokana na kitabu cha "al Fihrist". Katika kitabu hicho Ibn Nadeem aliarifisha taaluma na elimu zote zilizokuwepo katika zama hizo na kutoa maelezo na wasifa wa wasomi mashuhuri wa elimu hizo.

Kitabu hicho kinakusanya maelezo kamili kuhusu maulamaa na wasomi wa Kiislamu wa zamani hadi kufikia zama za Ibn Nadeem.  

Katika siku kama ya leo miaka 209 iliyopita, ufalme wa siku mia moja wa Napoléon Bonaparte ulianza nchini Ufaransa baada ya Bonaparte kutoroka sehemu aliyokuwa amebaidishwa katika kisiwa cha Elba.

Tarehe 27 mwezi Februari mwaka huohuo akiwa pamoja na wanajeshi elfu moja Napoleon Bonaparte alifanikiwa kutoroka katika kisiwa cha Elba ambako alikaa akiwa uhamishoni kwa kipindi cha miezi kumi na kurejea Ufaransa na utawala wa kifalme ukaanza nchini humo.   

Napoléon Bonaparte

Siku kama ya leo miaka 132 iliyopita yaani tarehe 1 Machi mwaka 1892, alizaliwa mjini Tokyo mwandishi na mtaalamu mkubwa wa Japan anayejulikana kwa jina la "Rhunosuke Akutagawa".

Mwandishi huyo anahesabika kuwa mmoja wa waasisi wa kanuni mpya za fasihi huko Japan. Akutagawa ameacha athari muhimu ikiwa ni pamoja na vitabu vya "Binti wa Buibui" na "Tushi Gun."

Mwandishi huyo alifariki dunia mwaka 1927.   

Rhunosuke Akutagawa

Miaka 126 iliyopita katika siku kama leo, kisiwa cha Puerto Rico kilichoko katika ya Bahari ya Atlantic kaskazini mwa Amerika ya Kusini, kilikaliwa kwa mabavu na vikosi vya majeshi ya Marekani baada ya kumalizika vita vya kikoloni vya Uhispania na Marekani.

Baada ya Marekani kukitwaa kwa nguvu kisiwa hicho ilikifanya ghala kubwa la silaha, kiasi kwamba Marekani iliasisi kambi 13 za kijeshi kisiwani humo.

Kisiwa hicho ambacho mara kwa mara hukumbwa na ukosefu wa amani, miongoni mwa nchi zinazozungumza lugha ya Kihispania katika bara la America.    

Kisiwa cha Puerto Rico

 

Tags