May 16, 2022 07:04 UTC
  • Wasichana katika sekta ya teknolojia

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala hii ambayo huangazia baadhi ya mafanikio katika uga wa sayansi, tiba na teknoloaji nchini Iran na maeneo mengine duniani. Ni matumaini yangu kuwa mtaweza kunufaika katika makala hii ya 151

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wasichana katika tasnia ya Habari na teknolojia ya mawasiliano ICT muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU umesema fursa na usalama mtandaoni ambayo ndio maudhui ya siku ya mwaka huu ni ufunguo wa kukiingiza kizazi kijacho cha wasichana katika Habari na teknolojia ya mawasiliano.

Kwa mujibu wa ITU maudhui hayo yanaonyesha nia ya pamoja ya dunia katika kuwawezesha vijana na wasichana kufaidika kwa usalama kutokana na maisha ya kidijitali. 

ITU inatambua haja ya kuhakikisha wasichana na wanawake wanafurahia fursa sawa za kujifunza kidijitali, hasa katika nchi zinazoendelea. 

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za ITU, duniani kote, asilimia 57 ya wanawake ndio wanatumia Intaneti  ikilinganishwa na asilimia 62 ya wanaume.  

Na duniani kote ni asilimia 30 tu ya wataalamu wa sayansi ya teknolojia na tasnia ya teknolojia ni wanawake.  

Ikiwa wanawake hawawezi kufikia mtandao na hawajihisi salama mtandaoni, hawawezi kukuza ujuzi muhimu wa kidijitali na kujihusisha katika nafasi za kidijitali, jambo ambalo linapunguza fursa zao za kuingia katika tasnia za teknolojia, uhandisi na hisabati au STEM. 

Doreen Bogdan-Martin, ni mkurugenzi wa kitengo cha maendeleo ya mawasiliano wa ITU. Anasema: "Ulimwenguni kote, wasichana na wanawake wanataka kujiunga na mapinduzi ya kidijitali. Tunapoondoa vikwazo vya fursa za ufikiaji na usalama, wanawake na wasichana wanaweza kutoa mchango mkubwa na kuwezeshwa na ICT. Kwa kifupi teknolojia inahitaji wasichana, na wasichana wanaihitaji teknolojia," 

Hivyo amesesisitiza kuwa,“Kwenye siku hii ya wasichana katika ICT hebu tufanye kazi pamoja kuhakikisha kwamba kila msichana na kila mwanamke kila mahali anapata fursa ya kutumia teknolojia ya kidigitali kustawi, kutimiza ndoto zake na kuwa katika ubora wake.” 

Naye Katibu Mkuu wa ITU Houlin Zhao katika ujumbe wake wa siku hii amesema: “Siku ya wasichana katika ICT ni wito wa kuchukua hatua kuhamasisha kizazi kijacho cha vijana wa kike na wasichana kuingia katika taaluma ya STEM, natoa wito kwa viongozi wote wa serikali, wafanyabiashara, vyuo vikuu na wengine kufanya kila wawezalo kusaidia vijana wa kike na wasichana na kuwapa nafasi ya kutimiza ndoto zao." 

Siku ya kimataifa ya wasichana katika ICT huadhimishwa kila mwaka katika Alhamisi ya mwisho ya mwezi Aprili na hadi kufikia leo zaidi ya wasichana na wanawake 600,000 wameshirikia hafla zaidi ya 12,000 za wasichana katika ICT katika nchi 195 kote duniani. 

Iran na Russia kushirikiana kiteknolojia

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia zimeanzisha kituo cha pamoja cha teknolojia kwa ajili ya kuendesha miradi ya pamoja ya ustawi na maendeleo katika uga huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, nchi mbili za Iran na Russia zina uwezo mkubwa wa kisayansi na kitekonolojia pamoja na ubunifu wa mambo mbalimbali hivyo mashirika ya teknolojia ya Iran yameamua kushirikiana na mashirika kama hayo ya nchini Russia kwa ajili ya kubadilishana uzoefu, kuuziana teknolojia na pia kusafirisha nje bidhaa na huduma za kiteknolojia ambazo ni uvumbuzi wa mara ya kwanza wa nchi hizo mbili ambao haujafanyika sehemu nyingine yoyote duniani. 

Kituo hicho kimefungliwa katika Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Saint Petersburg huko Russia kwa lengo la kutia kasi maendeleo ya kisayansi na kitekonolojia ya nchi hizo mbili.

Chuo hicho cha Russia ni katika vyuo vikuu vya daraja la kwanza duniani na sasa kinasimamia na kuendesha miradi kadhaa ya kitaifa ya teknolojia ya kisasa.

Kituo hicho cha pamoja cha teknolojia cha Iran na Russia kina uongozi wa kujitegemea na kina kumbi za pamoja kubwa za kuendesha semina na vikao mbalimbali na pia kina nafasi ya kuendesha masomo ya pamoja ya teknolojia. Kimetengewa nafasi pia ya kuimarisha mashirika ya elimu msingi pamoja na masuala ya uvumbuzi na ubunifu katika sekta tofauti zenye manufaa kwa mataifa haya mawili na duniani kwa ujumla.

Apu ya mHealth nchini Kenya

Kwa mujibu wa Mpango wa Ustawi wa 2030, sekta ya afya ya Kenya itazingatia utoaji huduma za kimatibabu kupitia njia za kidijitali.

Mkurugenzi wa Utoaji Huduma za Kimatibabu katika Wizara ya Afya ya Kenya, Dkt Kioko Jackson amesema “Kenya inalenga kutoa huduma bora, kwa gharama ya chini na kwa kila mtu katika mpango wake wa ustawi kufikia 2030. Ikiwa tutaendelea kutumia programu za kidijitali, basi tutaweza kutimiza hata kabla ya mwaka huo kufika."

Katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya programu za kidijitali maarufu kama mHealth yameongozeka.

Hii ni kwa sababu ya upenyezaji wa hali ya juu wa rununu au simu za mkononi na ufikiaji wa mtandao, kwa hivyo, mHealth ni mojawapo ya maeneo ya kimkakati ya kuzingatiwa katika utekelezaji wa Mkakati wa Afya wa nchi wa 2016-2020.

Mfumo wa afya nchini unaendelea kuimarika huku baadhi ya kaunti 47 zikikumbatia utoaji huduma za kimatibabu kidijitali.

Kitengo cha mHealth, kwa kushirikiana na Chama cha Taarifa za Afya nchini (KeHIA), pia kinaongoza katika utekelezaji wa miradi mipya ya kitaifa kama vile uundaji wa programu ya kuhifadhi maelezo ya kibinafsi ya mgonjwa, taarifa kamili kuhusu aina ya ugonjwa anayougua mhusika na kuanzisha mfumo wa uidhinishaji wa Mifumo ya Taarifa za Afya (HIS).

Baadhi ya idara za afya ambazo zimekumbatia mfumo wa kidijitali ni Idara ya Kutathmini Kiwango cha Ugonjwa (CCC) ambayo inatumia kompyuta kwa asilimia 88 kutoa huduma.

Kadhalika, Idara ya malipo inatumia mfumo wa kidijitali kwa asilimia 26. Hata hivyo, kuna haja kwa hospitali au vituo vya afya kukumbatia mfumo wa kidijitali hasa katika kufuatilia hali ya wagonjwa waliolazwa.

Huduma zinazotolewa kupitia programu hizo ni upendekezaji wa tiba na ushirikiano wa mawasiliano ya karibu kati ya mgonjwa na daktari wake.

Kadiri simu za rununu na programu mbalimbali za kutolea huduma za kimatibabu zinavyozinduliwa, wengi sasa wameanza kuchangamkia huduma za kimatibabu kidijitali.

Lengo la jumla la viwango vya mHealth nchini Kenya ni kuhakikisha muundo, maendeleo na utekelezaji wa masuluhisho ya mHealth yanayoshirikiana, yanayoweza kupanuka na endelevu ambayo yanawanufaisha wateja na wahudumu wa afya kwa njia ya umoja na ya kiujumla kwa matokeo bora ya afya.

Anaposajiliwa katika programu husika ya kidijitali, baadhi ya maelezo muhimu yanayofaa kujumuishwa ni majina, namabari ya simu, umri, jinsia, miaka, anakoishi na jina la kituo cha afya husika.

Kama njia ya kuimarisha sekta ya utoaji huduma za kimatibabu kidijitali, Shirikisho la Wahudumu wa Afya nchini (KMA) liliweza kusaini mkataba wa kushirikiana na shirika la Smart Applications International.

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wasichana katika tasnia ya Habari na teknolojia ya mawasiliano ICT muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU umesema fursa na usalama mtandaoni ambayo ndio maudhui ya siku ya mwaka huu ni ufunguo wa kukiingiza kizazi kijacho cha wasichana katika Habari na teknolojia ya mawasiliano.

Kwa mujibu wa ITU maudhui hayo yanaonyesha nia ya pamoja ya dunia katika kuwawezesha vijana na wasichana kufaidika kwa usalama kutokana na maisha ya kidijitali. 

ITU inatambua haja ya kuhakikisha wasichana na wanawake wanafurahia fursa sawa za kujifunza kidijitali, hasa katika nchi zinazoendelea. 

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za ITU, duniani kote, asilimia 57 ya wanawake ndio wanatumia Intaneti  ikilinganishwa na asilimia 62 ya wanaume.  

Na duniani kote ni asilimia 30 tu ya wataalamu wa sayansi ya teknolojia na tasnia ya teknolojia ni wanawake.  

Ikiwa wanawake hawawezi kufikia mtandao na hawajihisi salama mtandaoni, hawawezi kukuza ujuzi muhimu wa kidijitali na kujihusisha katika nafasi za kidijitali, jambo ambalo linapunguza fursa zao za kuingia katika tasnia za teknolojia, uhandisi na hisabati au STEM. 

Doreen Bogdan-Martin, ni mkurugenzi wa kitengo cha maendeleo ya mawasiliano wa ITU. Anasema: "Ulimwenguni kote, wasichana na wanawake wanataka kujiunga na mapinduzi ya kidijitali. Tunapoondoa vikwazo vya fursa za ufikiaji na usalama, wanawake na wasichana wanaweza kutoa mchango mkubwa na kuwezeshwa na ICT. Kwa kifupi teknolojia inahitaji wasichana, na wasichana wanaihitaji teknolojia," 

Hivyo amesesisitiza kuwa,“Kwenye siku hii ya wasichana katika ICT hebu tufanye kazi pamoja kuhakikisha kwamba kila msichana na kila mwanamke kila mahali anapata fursa ya kutumia teknolojia ya kidigitali kustawi, kutimiza ndoto zake na kuwa katika ubora wake.” 

Naye Katibu Mkuu wa ITU Houlin Zhao katika ujumbe wake wa siku hii amesema: “Siku ya wasichana katika ICT ni wito wa kuchukua hatua kuhamasisha kizazi kijacho cha vijana wa kike na wasichana kuingia katika taaluma ya STEM, natoa wito kwa viongozi wote wa serikali, wafanyabiashara, vyuo vikuu na wengine kufanya kila wawezalo kusaidia vijana wa kike na wasichana na kuwapa nafasi ya kutimiza ndoto zao." 

Siku ya kimataifa ya wasichana katika ICT huadhimishwa kila mwaka katika Alhamisi ya mwisho ya mwezi Aprili na hadi kufikia leo zaidi ya wasichana na wanawake 600,000 wameshirikia hafla zaidi ya 12,000 za wasichana katika ICT katika nchi 195 kote duniani. 

Google yawekeza Kenya

Kampuni kubwa ya mtandaoni ya Google imetangaza hivi karibuni kuwa itafungua kituo chake cha kwanza cha kutengeneza bidhaa barani Afrika kitakachokuwa na makao yake katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Kampuni hiyo yenye makao yake mjini Mountain View California, nchini Marekani inapanga kuwekeza dola bilioni moja katika miaka mitano ijayo ili kulenga soko la mtandaoni linalokuwa kwa kasi katika bara hilo.

Google inataka kupata sehemu kubwa zaidi kwenye soko linalopanuka la watu wanaotumia mtandao barani Afrika ambao wanatarajia kufikia milioni 800 ifikapo mwaka 2030.

Kampuni hiyo inaanzisha kituo chake cha kutengeneza bidhaa jijini Nairobi ambacho kimepangwa kufunguliwa mwaka 2023 na kitaajiri zaidi ya watu 100. Kampuni hiyo ya teknolojia ya kimataifa ilisema malengo yake ni kufanya habari za ulimwengu zipatikane na watu wote na kubuni bidhaa ambazo zinafanya kazi vyema kwa wa-Afrika.  Wakati huo huo Microsoft pia hivi karibuni iliwekeza nchini Kenya kwa kuzindua kituo kilichogharimu dola milioni 27.