Aug 03, 2021 06:06 UTC
  • Elias Kwandikwa,Waziri wa Ulinzi wa  Tanzania afariki dunia

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania, Elias Kwandikwa, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ulinzi wa Tanzania, alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa karibu siku kumi na nne.

Haijabainishwa maradhi aliyokuwa akiugua Kwandikwa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la  Ushetu katika mkoa wa Shinyanga.

Katibu wa Mbunge huyo, Julius Lugobi amethibitisha kuwa Mbunge huyo ameaga dunia hapo jana.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole na rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini humo, Jenerali Venance Mabeyo, Taarifa kutoka Ikulu imeeleza.

Rais Samia amesema katikka ujumbe wake huuo wa salamu za rambirambi kkwamba, amepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha waziri huyo kutokana na mchango wake mkubwa katika utumishi wa Umma.

‘’Tumepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi wa Umma hautasahaulika, Kwandikwa alikuwa kiongozi shupavu ambaye alikuwa akitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu’’ amesema Rais Samia katika ujumbe wake huo

Hadi sasa haijabainishwa chanzo cha kifo cha waziri huyo wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa nchini Tanzania. Elias . Kwandikwa aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulizni Disemba mwaka jana na aliyekuwa Rais wa nchhi hiyo Johh Pombe Magufuli.