Aug 01, 2021 12:34 UTC
  • Familia za wahanga wa mauaji ya kimbari ya Tulsa wataka kufanyike uchunguzi wa mauaji hayo

Familia za Wamarekani weusi waliouawa kwa umati katika mji wa Tulsa kwenye jimbo la Oklahoma nchini Marekani zimetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu jinai hiyo na kuchukuliwa hatua wahusika wa mauaji hayo.

Ripoti iliyotolewa na gazeti la Guardian la Uingereza imeashiria maziko ya maiti 19 za wahanga wa muaji ya kimbari ya Tulsa  huko Marekani na kusema kuwa, familia za wahanga wa mauaji hayo zinataka kufanyike uchunguzi kuhusu jinai hiyo na kuchukuliwa hatua waliohusika kwa njia moja au nyingine ya uhalifu huo.

Baadhi ya watu walioandamana wakati wa maziko ya maiti hizo 19 za baadhi wa wahanga wa mauaji ya Tulsa walitaka kucheleweshwa shughuli ya maziko mengine ya wahanga hao hadi pale uchunguzi kuhusu mauaji hayo ya kimbari utakapofanyika. Hata hivyo maafisa wa mji wa Tusla wamekaa wito huo. 

Miili ya wahanga hao 19 wa mauaji ya kimbari ya Tusla ilizikwa tena Ijumaa iliyopita bila ya kuhudhuriwa na familia za wahanga hao. 

Tarehe 31 hadi Mosi Mei mwaka 1921 wazungu wa Marekani waliopewa silaha za moto na maafisa wa serikali walishambulia makazi ya raia weusi katika wilaya ya Greenwood, mji wa Tulsa katika jimbo la Oklahoma na kuuwa watu zaidi 300 na kuacha wengine 10,000 wakiwa bila ya makazi. Wazungu hao walifanya uharibu mkubwa na kusawazisha kabisa mji huo na ardhi baada ya kuteketeza kila kitu. 

Mji huo wa Wamarekani weusi ulikuwa umestawi na kupiga hatua kubwa za maendeleo kiasi cha kujulikana kwa jina la Black Wall Street. Mashambulizi ya wabaguzi hao yalihaibu kabisa maduka makubwa ya biashara, maktaba, mahospitali, shule na kadhalika.

Hadi sasa hakuna hata manusura mmoja au familia ya wahanga wa mauaji ya umati ya Tulsa aliyepewa fidia kutokana na uhalifu huo wa kutisha, na makampuni ya bima ya Marekani yamekataa katakata kushugulikia kesi hiyo.

Katika hotuba yake ya mwezi uliopita kwenye kumbukumbu ya mwaka wa 100 tangu baada ya mauaji yaliyofanywa na wazungu dhidi ya Wamarekani weusi katika mji wa Tulsa jimboni Oklahoma, Rais Joe Biden wa Marekani aliutaja ugaidi wa wazungu wabaguzi wa rangi wanaojiona kuwa bora kuliko wanadamu wengine kuwa ni tishio hatari zaidi kwa Marekani. 

Mabaki ya mji wa Wamarekani weusi, Tulsa

Biden ambaye anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kutembelea eneo la mauaji ya umati ya mamia ya raia weusi wa nchi hiyo katika mji wa Tulsa yaliyofanyika miaka mia moja iliyopita, ameonya juu ya kuendelea kuwepo fikra za ubaguzi wa rangi nchini Marekani. 

Tags